Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Februari 08, 2025 Local time: 18:27

Mahakama ya kijeshi Uganda imepigwa marufuku kusikiliza kesi za kiraia


Mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda Dkt. Kiiza Besigye akiwa katika mahakama ya kijeshi
Mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda Dkt. Kiiza Besigye akiwa katika mahakama ya kijeshi

Mahakama ya juu nchini Uganda imeamuru kesi zote zinazowahusu raia katika mahakama ya kijeshi zisitishwe mara moja kusiskilizwa na zihamishwe hadi mahakama za kawaida.

Jopo la majaji saba wakiongozwa na Jaji mkuu Alfonse Owing Dollo limeamua kwamba mahakama ya kijeshi imeundwa kisheria lakini ina uwezo tu wa kusikiliza kesi zinazowahusu wanajeshi na wala sio raia.

Majaji wamesema kwamba hakuna uhakika kwamba mahakama za kijeshi ni huru kutekeleza kazi yake kisheria kwa sababu majaji wa mahakama hiyo ni wanajeshi na wameteuliwa na rais.

Uamuzi huo ni ushindi mkubwa kwa watetezi wa haki za binadamu ambao wamekuwa wakipinga hatua ya raia kufunguliwa mashtaka katika mahakama ya kijeshi.

Forum

XS
SM
MD
LG