Kenya inafanya juhudi za kuwaingiza wakimbizi katika jamii kabla ya mipango ya kufunga kambi ambazo zimekuwa zikiwapatia hifadhi zaidi ya watu 400,000 kutoka Somalia, Sudan Kusini na Congo.
Zaidi ya watu milioni nne wanakabiliwa na viwango vya juu vya ukosefu wa usalama wa chakula nchini Kenya kwa mujibu wa Data mpya zilizotolewa na Umoja wa Mataifa.
Tume ya uchaguzi nchini Kenya inasema ukaguzi unaoendelea katika daftari la wapiga kura umegundua kuwa kuna karibu wapiga kura 250,000 waliokufa ambao wameandikishwa.
Chama cha Wiper nchini Kenya kimewahakikishia wafuasi wake kiongozi wao Kalonzo Musyoka bado yuko katika kinyang’anyiro cha uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika Agosti 9, kinyume na ripoti za awali zilizoeleza kuwa amezuiliwa na Tume ya Uchaguzi, IEBC, kwamba alishindwa kutimiza baadhi ya masharti.
Kiongozi wa Chama cha Wiper nchini Kenya, Kalonzo Musyoka hatashiriki katika kinyang’anyiro cha uchaguzi wa Rais Agosti 9 baada ya tume ya uchaguzi ya nchi hiyo kumzuia kugombea kutokana na utaratibu uliopo.
Naibu Rais wa Kenya William Ruto amemuomba Rais Uhuru Kenyatta msamaha baada ya viongozi hao kutumbukia katika mvutano baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2018.
Pandisha zaidi