Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio, akizungumza kutoka Santo Domingo akiwa pamoja na Rais wa Dominican Republic Luis Abinader, alikiri kwamba kikosi hicho, kinachoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, hakiwezi kutatua mzozo wa sasa.
Magenge mabaya ya wahalifu, yenye silaha zinazosafirishwa kimagendo kutoka Marekani, yamekusanyika katika mji mkuu wa Haiti wa Port au Prince na sasa yanadhibiti eneo kubwa la mji huo. Magenge hayo yanadhibiti pia maeneo mengine kadhaa, yakiwemo maeneo ambako kilimo kinafanyika kwa wingi.
“Suluhisho la mzozo wa Haiti liko mikononi mwa wananchi wa Haiti, mikononi mwa wasomi wa Haiti, Rubio alisema.
“Lakini tutasaidia, hatuwezi kupuuza matatizo yaliyoko huko.”
Ujumbe huo wa kiusalama, ulioidhinishwa na Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lakini usioongozwa na Umoja wa Mataifa, umekabiliwa na changamoto katika juhudi za kupiga hatua katika kupambana na magenge hayo kwa sababu idadi ya maafisa wake wa usalama bado ni ndogo na inategemea michango ya hiari kutoka kwa mataifa wanachama.
Kikochi cha askari polisi wa Kenya 144 kiliwasili mjini Port-au Prince Alhamisi, huku Rais wa Kenya William Ruto akiongeza kuwa alizungumza na Rubio kuhusu kikosi hicho.
Umoja wa Mataifa ulionya wiki hii kwamba Marekani ilizuia zaidi ya dola milioni 13 za ufadhili kwa kikosi cha usalama ambazo ilikuwa imetoa kwa mfuko maalum wa Umoja wa Mataifa, kama sehemu ya hatua ya Rais Donald Trump ya kusitisha misaada yote ya kigeni kwa siku 90.
Forum