Kennes Bwire is a journalist with Voice of America and is based in Washington DC.
Serikali ya Haiti iliomba rasmi msaada wa usalama kutoka kwa nchi zote kote duniani, zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
Wanajeshi wawili wa Uganda wamelazwa hospitalini wakiwa katika hali mahtuti baada ya kupigwa risasi na kundi la waasi masahriki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
India na Tanzania zinatafuta namna ya kuendesha biashara kwa kutumia sarafu zake kutokana na uhaba wa dola duniani.
Mapigano makali yanaendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kati ya kundi lenye silaha linalojiita Wazalendo, ambalo linaungwa mkono na serikali na kundi la M23.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametuma ujumbe wa rambi rambi kwa familia na taifa kwa jumla, kufuatia kifo cha aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Benard Membe, aliyefariki dunia asubuhi leo Ijumaawakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Kairuki, mjini Dar-es-salaam.
Kamanda wa jeshi la jumuiya ya Afrika mshariki Meja Generali Jeff Nyagah amejiuzulu nafasi hiyo na kurudi Nairobi.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameanza kufanya mikutano na vigogo wa chama kinachotawala cha National resistance movement NRM kujua sababu zinazopelekea baadhi yao kupinga azma ya mtoto wake Generali Muhoozi Kainerugaba kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2026.
Waziri wa habari wa Uganda Dr. Chris Baryomunsi amesema kwamba rais Yoweri Museveni atasaini muswada uliopitishwa na bunge unaoharamisha ushoga nchini humo, na kuwa sheria.
Waasi wa M23 wameripotiwa kushambulia kambi ya wanajeshi wa Burundi waliowasili mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo siku chache zilizopita kwa ajili ya kulinda amani.
Msimamizi mkuu wa bajeti ya Kenya ameambia Bunge la nchi hiyo kwamba alikuwa akilazimishwa kutoa mabilioni ya pesa kwa maafisa wa serikali wakati utawala wa rais Uhuru Kenyatta ulikuwa unaelekea kumalizika.
Mswada unatayarishwa nchini Uganda kwa lengo la kuharamisha kabisa mapenzi ya jinsia moja, ukiwa na adhabu ya hadi miaka 10 gerezani na faini ya hadi shilingi milioni 10 za Uganda.
Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema kwamba yupo tayari kukabiliana na tishio lolote la kiusalama kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Waasi kutoka muungano wa makundi yanayolisaidia jeshi la serikali ya DRC wanaripoti kwamba wamewashinda nguvu na kuwafukuza waasi wa kundi la M23 kutoka Rubaya, baada ya kuudhibithi mji huo kwa muda mfupi.
Mapigano makali yanaendelea Kivu kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kati ya jeshi la serikali FARDC na waasi wa kundi la M23.
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ametishia kuongoza maandamano makubwa kote nchini humo iwapo serikali haitakuwa imehakikisha kwamba gharama ya maisha imeshuka ndani ya siku 14.
Uganda imesema kwamba ipo tayari kutuma wanajeshi wake mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupambana na kundi la waasi la M23.
Serikali ya Kenya imetangaza kwamba itatuma wanajeshi katika eneo la North Rift kupambana na wezi wa mifugo ambao wamehatarisha Maisha ya wakaazi wa sehemu hiyo na kushambulia maafisa wa usalama wa serikali.
Kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis, ametoa wito kwa makundi yanayopigana mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kuweka chini silaha kabisa na kukumbatia amani kwa ajili ya maendeleo ya taifa hilo.
Kiongozi wa kanisa Katoliki Papa Francis, ameyataka mataifa ya nje kuacha kupora mali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na bara la Afrika kwa jumla, ili kutosheleza tamaa yao.
Ndege za kijeshi za jamhuri ya kidemokrasia ya Congo zimeendelea kushambulia waasi wa kundi la M23 wanaoshikilia mji wa Kitchanga, Kivu kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Pandisha zaidi