Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 07:57

Kenya: Serikali ya Uhuru imedaiwa kuiba mabilioni ya pesa kabla ya kuondoka madarakani


Aliyekuwa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika mojawapo ya mikutano yake, Nairobi, Kenya, baada ya kuondoka madarakani. Dec. 6, 2022.
Aliyekuwa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika mojawapo ya mikutano yake, Nairobi, Kenya, baada ya kuondoka madarakani. Dec. 6, 2022.

Msimamizi mkuu wa bajeti ya Kenya ameambia Bunge la nchi hiyo kwamba alikuwa akilazimishwa kutoa mabilioni ya pesa kwa maafisa wa serikali wakati utawala wa rais Uhuru Kenyatta ulikuwa unaelekea kumalizika.

Mabilioni ya pesa zinadaiwa kutolewa siku chache kabla ya uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti na wakati kulikuwa na kesi mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi huo.

Kiasi kinachojulikana kufikia sasa ni shilingi bilioni 15.

Kulingana na vyombo vya habari vya Kenya, na vyanzo vya habari katika kamati ya bunge ya kusikiliza malalamishi ya uma inayoongozwa na Nimroid Mbai, msimamizi wa bajeti Margaret Nyakang’o ameambia kamati hiyo ya bunge kwamba alikuwa akilazimishwa kutoa mabilioni ya pesa kwa njia zisisofahamika.

Shilingi bilioni 15 zilitolewa kwa ofisi ya rais Uhuru Kenyatta, pamoja na wizara ya ujenzi, siku chache kabla ya uchaguzi mkuu.

Pesa pia zilikuwa zinatolewa kwa mazingira tatanishi wakati wa janga la virusi vya Corona.

Shilingi bilioni 1 zilitolewa April 1,2022 na kupelekwa kwa ofisi ya rais kwa kile kimertajwa kama sababu za kiusalama.

Agosti 4, siku chache kabla ya uchaguzi mkuu, shilingi bilioni 10 zilitolewa kwa waizara ya ujenzi.

Javas Bigambo, mtaalam wa utawala bora anasema kwamb sheria za Kenya zilivunjwa kwa pesa kutolewa pasipo idhini ya bunge la taifa.

Mawasiliano ya whatsapp kati ya waziri wa fedha na msimamizi wa bajeti

Nakala inayodaiwa kuwa ya mawasiliano kwa njia ya whatsapp, kati ya msimamizi wa bajeti na aliyekuwa waziri wa fedha Ukur Ytani, inaonyesha Yatani akimwelekeza msimamizi wa bajeti kutoka mabilioni ya pesa, ikiwemo kile kilielezwa kuwa changamoto za mafuta ya petroli.

Nakala hiyo pia ina mawasiliano yaliyoambatanishwa yanayodaiwa kuwa barua kutoka kwa benki kuu.

Katika mazungumzo yao, wanagusia pia mikutano na maelekezo kutoka kwa rais, pamoja na mkaguzi wa bajeti kuambiwa kutoa pesa kwa haraka kabla ya kupigiwa sim una rais.

Mojawapo ya maelekezo yanamtaka msimamizi ya bajeti kuruhusu kutolewa kwa shilingi bilioni 10 ndani ya muda wa dakika 26.

Mkaguzi wa bajeti ya serikali, amefichua hayo kwa kamati ya bunge siku chache baada ya naibu rais RIgathi Gachagua kudai kwamba maafisa katika serikali ya Uhuru Kenyatta waliiba pesa za serikali siku chache kabla ya kuondoka ofisini.

Wanasiasa wa upinzani wamefutilia mbali madai hayo wakidai kwamba ni njama za kuharibia sifa uliokuwa utawala wa rais Uhuru Kenyatta, na kutaka kupumbaza watu wasitambue kwamba utawala wa rais William Ruto umeshindwa kutekeleza ahadi zake.

Lakini naibu rais Gachagua ametishia kufichua majina ya wahusika wote, akidai kwamba zaidi ya shilingi bilioni 24 ziliibwa wakati kesi ya uchaguzi ilikuwa inasikilizwa mahakamani.

XS
SM
MD
LG