Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 17:16

Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa chasitisha safari zake za ndege

Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa kilichopo Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO) kikiwa katika helikopta eneo la Goma, jimbo la Kivu Kaskazini. Julai 26, 2022. Picha na Shirika la habari la REUTERS/Esdras Tsongo.

Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kimesitisha safari za ndege katika jimbo la Kivu Kaskazini, baada ya moja ya ndege zake kushambuliwa Ijumaa.

Msemaji wa safari za ndege za Umoja wa Matiafa na shirika la Chakula Duniani WFP Claude Kalinga, amesema kwamba safari za ndege kati ya Goma na miji ya mashariki mwa DRC ya Beni na Bunia zimesitishwa kwa muda usiojulikana.

Helikopta ya Umoja wa Mataifa ilishambuliwa kwa karibu dakika 10, Ijumaa Februari 24, nje ya mji wa Goma, ilipokuwa inarudi Goma kutoka Walikale.

Ndege hiyo ilifanikiwa kutua Goma, na wafanyakazi wake pamoja na abiria 10 walifika salama.

Kalinga amesema kwamba kundi lililoshambulia ndege hiyo halijatambuliwa na kwamba safari za ndege zitarejea baada ya kufanyika tathmini ya kina kuhusu hali ya usalama.

XS
SM
MD
LG