Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 17:06

Nigeria yaendelea kuhesabu matokeo ya uchaguzi wa rais wenye ushindani mkali


Maafisa wa uchaguzi wakikusanya matokeo kwenye kituo cha kupigia kura mjini Lagos, Februari 26, 2023
Maafisa wa uchaguzi wakikusanya matokeo kwenye kituo cha kupigia kura mjini Lagos, Februari 26, 2023

Nigeria pole pole imeendelea kuhesabu matokeo hivi leo Jumatatu baada ya uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali katika wadhifa wa urais kwenye taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika huku kukiwa na uchelewesho na shutuma ambazo zimechochea mivutano.

Karibu watu milioni 90 walipiga kura Jumamosi kumchagua mrithi wa Rais Muhammadu Buhari, huku wengi wakiwa na matumaini ya kumpata kiongozi mpya ambaye atashughulikia suala la ukosefu wa usalama, matatizo ya uchumi na umaskini uliokithiri.

Kinyang’anyiro cha urais kilikuwa kati ya gavana wa zamani wa Lagos Bola Tinubu, mwenye umri wa miaka 70, mgombea wa chama tawala cha All Progressives Congress (APC) na makamu rais wa zamani Atiku Abubakari mwenye umri wa miaka 76, mgombea wa chama cha Peoples Democratic Party (PDP).

Lakini kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa utawala wa kijeshi mwaka 1999, mgombea wa tatu aliyewashangaza wengi, Peter Obi wa chama cha Labor, ameonyesha ushindani wake kwa vyama vya APC na PDP kwa kupigiwa kura na vijana.

Ikitangaza matokeo ya awali ya majimbo, tume huru ya kitaifa ya uchaguzi (INEC), Jumapili ilisema mgombea wa APC, Tinubu alishinda kwa tofauti ya kura chache katika jimbo la kusini magharibi la Etiki, huku chama cha PDP kikichukua nafasi ya pili.

XS
SM
MD
LG