Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 29, 2024 Local time: 11:52

Upinzani DRC wadai kuna dosari katika zoezi la kuandikisha wapiga kura


Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felix Tshisekedi (Katikati).
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felix Tshisekedi (Katikati).

Baadhi ya wagombea wa upinzani huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameelezea wasi wasi wao juu ya uchelewesho na madai ya dosari katika zoezi la uandikishaji wapiga kura ambapo wamesema linafanywa  kuwakandamiza wapinzani katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Desemba mwaka huu.

Hadi kufikia tarehe 17 Machi zaidi ya wapiga kura milioni 50 nchini Kongo wanatarajiwa kuandikishwa, lakini tume ya uchaguzi ya CENI Ijumaa ilisema baadhi ya vituo ambavyo haikuvitaja katika eneo la kwanza la usajili katika majimbo 10 ukiwemo mji mkuu Kinshasa vilivuka muda uliowekwa na tayari muda huo umeongezewa kwa siku 25.

“ Watapewa muda wa kufidia” afisa habari wa CENI Patricia Nseya alisema katika taarifa yake iliyotaja matatizo ya uendeshaji wa zoezi hilo bila kutoa maelezo zaidi.

Vituo 24 katika jimbo la Kinshasa na vingine ambayo idadi kamili haijulikani vya jimbo la Mai Ndombe havijafunguliwa kwa sababu za kiusalama.

Nyaraka ya ndani ya CENI ambayo shirika la habari la Reuters imeipata, inaonyesha kuwa mpaka tarehe 2 Februari vituo 779 kati ya vituo vya 9,200 vya kanda ya kwanza ya usajili vilifungwa au havikuwa vikifanya kazi na asilimia 52 tu ya wapiga kura wameandikishwa.

Wakizungumza na shirika la habari la Reuters, raia watatu wa Kongo na wataalam wa kimataifa wa uchaguzi, ambao hawakutaka majina yao kutajwa, pia wamesema wamekuwa wakiona tofauti kati ya vifaa vya usajili katika maeneo yanayomuunga mkono Tshisekedi na yale ya upinzani.

XS
SM
MD
LG