Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 26, 2024 Local time: 11:14

Ethiopia yafanya mashambulizi ya pili ya anga Tigray


Jeshi la anga la Ethiopia lashambulia tena Tigray
please wait

No media source currently available

0:00 0:01:07 0:00

Jeshi la anga la Ethiopia lashambulia tena Tigray

Ethiopia imefanya mashambulizi ya pili ya anga wiki hii katika mji mkuu kwenye mkoa wa Tigray.

Shambulizi hilo la Jumatano linaendeleza kampeni ya kupunguza nguvu vikosi vya Tigray katika vita vilivyodumu kwa takriban mwaka mmoja.

Televisheni ya Tigray inayosimamiwa na Tigray People's Liberation Front, imesema mashambulizi yalilenga katikati mwa Mekele lakini haikutoa maelezo zaidi ya majeruhi au uharibifu.

Imeonyesha picha ya kitu kama moshi na kusema katika ujumbe wa Facebook kwamba shambulizi lilifanyika majira ya saa nne asubuhi kwa saa za Ethiopia.

Hata hivyo baadae serikali ya Ethiopia ilisema shambulizi lililenga majengo ambako wapiganaji wa vikosi vya Tigray walikuwa wanatengeneza silaha.

Vikosi hivyo vimesema shambulizi linaonyesha kukata tamaa kwa serikali.

Pande hizo mbili zimekuwa zikipigana vita kwa takriban mwaka mmoja sasa ambavyo vimesababisha vifo vya maelfu ya watu na kukosesha makazi wengine milioni mbili.

XS
SM
MD
LG