Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 09:54

HRW yaripoti vitendo vya ubakaji na mauaji dhidi ya wakimbizi wa Eritrea


Ripoti ya HRW yaonyesha mauaji na ubakaji dhidi ya wakimbizi wa Eritrea
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:48 0:00

Ripoti ya HRW yaonyesha mauaji na ubakaji dhidi ya wakimbizi wa Eritrea

Shirika la Haki za Binadamu - Human Rights Watch, limesema wakimbizi wa Eritrea waliojikuta katika vita vya miezi kadhaa nchini Ethiopia wamekumbwa na unyanyasaji ikiwemo kunyongwa na ubakaji ambavyo ni sawa na uhalifu wa vita.

Ripoti mpya kutoka shirika hilo lenye makao yake Marekani imeonyesha mchango wa pande zote mbili za wanajeshi wa Eritrea na wapiganaji waasi kutoka mkoa wa kaskazini mwa Ethiopia, Tigray.

Familia zikiombeleza vifo vya wahanga wanaodaiwa waliuawa na wanajeshi wa Eritrea katika kijiji cha Dengolat, Kaskazini Mekele, Tigray Feb. 26, 2021.
Familia zikiombeleza vifo vya wahanga wanaodaiwa waliuawa na wanajeshi wa Eritrea katika kijiji cha Dengolat, Kaskazini Mekele, Tigray Feb. 26, 2021.

Inaeleza pande hizi mbili zilichangia katika mauaji makubwa yaliyosababishwa na ghasia baada ya wakimbizi kulazimishwa kuhama kwa nguvu na uharibifu mkubwa katika kambi mbili za wakimbizi.

Mkurugenzi wa human rights watch katika pembe ya afrika Letitia Bader amesema mauaji ya kutisha, ubakaji na uporaji dhidi ya wakimbizi wa Eritrea huko Tigray ni uhalifu wa vita wa wazi.

kwa miaka mingi Tigray ilikuwa makao salama kwa raia wa Eritrea waliokimbia unyanyasaji lakini hivi sasa wengi wanaona hawako salama.

Ghasia zilizuka kaskazini mwa Ethiopia novemba mwaka jana wakati Waziri mkuu Abbey Ahmed alipotuma wanajeshi huko Tigray kukiondoa chama tawala na uongozi wa TPLF, hatua aliyosema ilisababisha uvamizi katika kambi za jeshi la serikali.

XS
SM
MD
LG