Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 22, 2025 Local time: 21:25

Mitandao ya kijamii ilivyogeuka uwanja wa vita katika mgogoro wa Tigray


FILE - Kifaru kilivyoharibiwa wakati wa vita kati ya majeshi ya ulinzi ya Ethiopia na Vikosi Maalum vya Tigray nje ya mji wa Humera, Ethiopia, Julai 1, 2021. REUTERS/Stringer/File Photo
FILE - Kifaru kilivyoharibiwa wakati wa vita kati ya majeshi ya ulinzi ya Ethiopia na Vikosi Maalum vya Tigray nje ya mji wa Humera, Ethiopia, Julai 1, 2021. REUTERS/Stringer/File Photo

Wakati majeshi ya serikali kuu ya Ethiopia na kikundi cha Tigray People’s Liberation Front (TPLF) yalipoanza mapigano Novemba 2020, mapambano mengine yakajitokeza katika mtandao, ambapo pande zote zilikuwa zinataka kudhibiti maelezo ya vita hivyo.

Mitandao ya kijamii ikawa ni uwanja wa vita, huku serikali ya Ethiopia na wafuasi wake wakiwa upande mmoja na wanaharakati wa Tigray na wafuasi wao wakiwa upande mwingine.

Kila upande ulijaribu kuelezea vile hali ilivyokuwa kwa wasikilizaji wao wanaozungumza Kiingereza, kwa mujibu wa mtandao wa The Media Manipulation Casebook.

Ikiwa kimeanzishwa na kituo cha teknolojia cha Shorenstein na mradi wa Social Change katika Shule ya Harvard Kennedy, kikundi hicho cha Casebook kimekuwa kikifanya utafiti juu ya kampeni zinazohusiana na taarifa za Tigray tangu kuanza kwa vita.

Upande wa Tigray umejikita zaidi katika kuongeza uelewa juu ya vita hivyo, wakati wafuasi wa utawala wa Waziri Mkuu Abiy Ahmed mjini Addis Ababa unatafuta kukanusha madai ya mahasimu wao.

Wakati pande zote zinatoa madai ya upotoshaji au ya uongo, tafiti hiyo imegundua kuwa mawasiliano rasmi na habari zinazobandikwa za kuiunga mkono serikali mara nyingi zinatafuta njia ya kuzitia dosari habari zinazokinzana na maelezo ya serikali kuu kuwa ni zenye upotoshaji.

“Hii ni hali yenye mkanganyiko na siasa za eneo la Pembe ya Afrika, madhila ya kihistoria, uanaharakati, kauli za chuki, habari potofu, ushawishi katika safu na propaganda, yote yakitokea katikati ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea huko,” hii ni kwa mujibu wa tafiti iliyofanywa na Media Manipulation Casebook.

Wakati ilipoanza vita, wanaharakati wa Tigray waliitumia Twitter, na kikundi cha watetezi kisicho kuwa cha kibiashara Stand With Tigray kilianzishwa.

Wakati huohuo, vikundi vinavyounga mkono serikali kama vile Ethiopia State of Emergency Fact Check vilijaribu kukabiliana na kile walichokiona ni upotoshaji wa taarifa unaofanywa na TPLF, ikiwa mara nyingi unaonyesha habari za ndani na nje zina dosari.

Wakiendesha operesheni yao katika Twitter na Facebook peke yake, kikundi hicho, ambacho kilijibadilisha na kujiita Ethiopia Current Issues Fact Check (ECIFC), kimejitokeza na matamko na taarifa nzito ambazo zimekuwa zikilaani habari za kimataifa juu ya vita hivyo.

Baadhi ya wachambuzi waliohojiwa na VOA wanaamini kuwa serikali kuu ilianzisha kikundi hicho. Mamlaka zinakanusha madai hayo, na wanaounga mkono serikali wanaiona ECIFC kuwa ni muhimu kwa ajili ya kujibu kile wanachokiona ni upotoshaji unaofanywa na vyombo vya habari kuhusu vita hiyo.

“Utoaji habari umetekwa na wanaofungamana na TPLF ambao wanaishi mbalimbali katika mataifa ya Magharibi,” Dina Mufti, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ethiopia ameiambia VOA.”

Hawa wanaoendesha vikundi hivi ndio ambao hasa wanaotoa taarifa potofu na kampeni zisizokuwa na ukweli. Na hawaisaidii jamii ya kimataifa kufahamu ukweli uliovyo katika medani ya vita.”

Deacon Yoseph Tafari, mwenyekiti wa Baraza la Kiraia la Wamarekani wenye asili ya Ethiopia, jumuiya inayojieleza yenyewe kama ni watetezi wa haki za binadamu na utawala wa kisheria nchini Ethiopia, wanakubali hilo.

“Lazima ilitakiwa kifanyike kitu,” ameiambia VOA, akieleza kile anachokiona kuwa ni ripoti zinazoelemea upande moja. “Katika hali kama hii, serikali haina njia nyingine au vitendea kazi vingine inavyomiliki.”

Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari

XS
SM
MD
LG