Wakati Ahmed akiimarisha nguvu zake ndani ya nchi kumekuwa na ongezeko la wasiwasi wa kimataifa kwa serikali yake namna inavyoshughulikia mzozo kaskazini mwa Ethiopia.
Chama cha Abbiy kilipata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa Juni.
Aliapishwa Jumatatu na sherehe ilifanyika baadae katika mji mkuu Addis Ababa, iliyohudhuriwa na wakuu kadhaa wa nchi za Kiafrika.
Rais Sahle-Work Zewde aliliambia bunge leo Jumatatu kwamba vipaumbele vya serikali, ni pamoja na kupunguza mfumuko wa bei, ambao umepanda na kufikia karibu asilimia 20 mwaka 2021.Vingine ni gharama ya maisha, pamoja na kupunguza uosefu wa ajira.
Umoja wa Mataifa unaonya kwamba maelfu ya watu wanakabiliwa na njaa katika mkoa wa kaskazini wa Tigray, uliokumbwa na vita nchini Ethiopia.
Mgogoro ulizuka huko miezi 11 iliyopita, kati ya wanajeshi wa serikali na vikosi vitiifu vya Tigrayan People’s Liberation Front (TPLF), chama cha kisiasa kinachodhibiti Tigray.
Maelfu wamekufa na zaidi ya watu million mbili wamelazimika kukimbia makazi yao.