Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 12:52

Uchaguzi uliocheleweshwa wafanyika katika majimbo matatu Ethiopia


Waziri Mkuu Abiy Ahmed
Waziri Mkuu Abiy Ahmed

Waethiopia katika majimbo matatu ambapo uchaguzi ulikuwa umecheleweshwa wanachagua wawakilishi wao Alhamisi.

Wakati huohuo jimbo moja likipiga kura ya kuamua ikiwa litakuwa huru kutoka serikali kuu.

Shirika la habari la Reuters linaripoti kwamba Waziri Mkuu Abiy Ahmed ataunda serikali ijayo bila kujali matokeo ya kura hiyo iliyochelewa.

Chama chake tayari kilishinda viti 410 kati ya viti 436 vya wabunge ambavyo viligombaniwa katika uchaguzi wa mwezi Juni.

Abiy yuko chini ya shinikizo la kimataifa juu ya vita katika mkoa wa kaskazini wa Tigray.

Mzozo ulizuka mnamo Novemba 2020, ukigawanya vikosi vya serikali kuu na vile vya washirika dhidi ya vikosi vilivyofungamana na Tigrayan People's Liberation Front (TPLF), ambayo ilidai kuchukua udhibiti wa Tigray baada ya miezi kadhaa ya vita, na umwagikaji wa damu.

Umoja wa Mataifa unasema sehemu za Tigray zinakabiliwa na njaa.

Kura ya Alhamisi inafanyika katika majimbo ya Somali, Harar, na lile la SNNPR.

XS
SM
MD
LG