Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 27, 2024 Local time: 02:39

Maafisa wa UN waliyofukuzwa Ethiopia waondoka


Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed muda mfupi baada ya kuapushwa kwa muhula wa pili Jumatatu
Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed muda mfupi baada ya kuapushwa kwa muhula wa pili Jumatatu

Maafisa saba wa mashirika ya Umoja wa mataifa ya kibinadamu waliofukuzwa nchini Ethiopia hawako tena nchini humo, Umoja wa mataifa umesema Jumatatu.

Msemaji wa Umoja wa mataifa Farhan Haq amesema “ waliondolewa nchini humo ili kuhakikisha usalama wao”.

Alhamisi, serikali ya waziri mkuu Abiy Ahmed iliwapa saa 72 maafisa hao wawe wameondoka Ethiopia. Serikali ilidai walikuwa wanaingilia masuala ya ndani ya nchi, na kuongeza tuhuma nyingine dhidi yao, ikiwemo kupeleka misaada na vifaa vya mawasiliano ya simu kwa waasi wa Tigray People’s Liberation Front ( TPLF).

Alhamisi, katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres alielezea mshtuko wake, wakati wa taarifa hiyo, na Ijumaa alizungumza moja kwa moja na Abiy.

Maafisa waliyofukuzwa ni pamoja na naibu mkuu wa Umoja wa mataifa wa masuala ya misaada ya kibinadamu, naibu mratibu wa misaada ya kibinadamu, na mwakilishi wa shirika la Umoja wa mataifa linalohudumia watoto ( UNICEF).

Umoja huo umesema kwamba, Ethiopia haina msingi wa kisheria wa kufukuza wafanyakazi wake.

XS
SM
MD
LG