Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 16:47

Mkuu wa idara ya uhamiaji UN Ethiopia asimamishwa kazi


Idara ya uhamiaji ya Umoja wa Mataifa, imempa likizo isiyo na malipo kiongozi wa idara hiyo wa Ethiopia, Maureen Achieng.

Hiyo ni kutokana na kufanya mahojiano kinyume na utaratibu ambapo alilalamika kutengwa na uongozi wa juu wa Umoja wa Mataifa.

Vilevile amesema uongozi wa UN ulikuwa na huruma na Watigrinya wanaotaka kujitenga.

Kuondoka kwa Maureen Achieng, kumethibitishwa katika barua anbayo shirika la habari la AFP iliiona.

Hali hii inatishia ufikishwaji wa misaada ya kibinadamu ambayo tayari ulizoroteshwa na uamuzi wa mwezi uliopita wa Ethiopia kuwafukuza viongozi saba wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kwa madai kuwa waliingilia masuala ya Ethiopia.

Tukio hili limetokea ikiwa ni miezi 11 imepita toka kuanza kwa vita vikali kaskazini mwa Ethiopia.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, vita hivyo vimesababisha maelfu ya watu kuingia katika hali ya baa la njaa.

Wiki iliyopita mahojiano ya Achieng na afisa mwingine wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa yalisambaa katika mitandao ya kijamii.

Alisikika akihojiwa na Jeff Pearce, ambaye amesha chapisha taarifa nyingi akiunga mkono hatua za serekali ya Ethiopia katika vita dhidi ya kundi la wanaotaka kujitenga Tigray - TPLF.

XS
SM
MD
LG