Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 20:45

Mapigano makali yaripotiwa kuendelea huko Tigray


Kifaru kikiwa kimeharibiwa wakati wa mapigano majeshi ya serikali ya Ethiopia na vikosi maalum vya Tigray nje ya mji wa Humera, Ethiopia, July 1, 2021.

Mapigano makali yanaripotiwa kuendelea katika jimbo la kaskazini mwa Ethiopia la Tigray wapiganaji wa TPLF wakisema serikali ilianzisha mashambulizi  ya anga Mekelle

Mapigano makali yanripotiwa kuendelewa katika jimbo la kaskazini mwa Ethiopia la Tigray ambapo wapiganaji wa kundi la TPLF kwa mara nyingine tena wakisema kwamba serikali ya Ethiopia ilianzisha mashambulizi ya anga kwenye mji mkuu wa Mekelle.

Mashambulio hayo ya mabomu yaliripotiwa pia na wakazi na wafanyakazi wa huduma za dharura huko Tigray, lakini serikali ya Ethiopia ilikana madai hayo.

Inaripotiwa kwamba watoto watatu wameuliwa na mtu mmoja kujeruhiwa kutokana na mashambulio hayo ya jana.

Umoja wa Mataifa ulisema unafuatilia ripoti za mashambulio hayo na msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric anasema wanawasi wasi mkubwa kutokana na athari zinazowakumba raia wa jimbo hilo.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Ned Price alisema Marekani pia inafuatilia habari za shambulio hilo akisema wana wasiwasi mkubwa na kile ambacho kimekuwa kuongezeka kwa vurugu huko Tigray kwa muda sasa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG