Taiwan imepigwa na matetemeko kadhaa ya ardhi saa kadhaa kati ya Jumatatu jioni na Jumanne asubuhi, karibu wiki tatu baada ya watu 17 kuuwawa kwenye tetemeko jingine la ardhi lenye ukubwa wa 7.4 kwa vipimo vya rikta.
Vyombo vya habari vya Marekani vimesema kuwa Israel imefanya mashambulizi ya anga nyakati za alfajiri ndani ya Iran Ijumaa vikiwanukuu maafisa wa Israel na Marekani ambao hawakutajwa majina.
Israeli ilifanya shambulizi la kombora Ijumaa alfajiri ndani ya Iran, vyombo vya habari vya Marekani viliripoti, vikiwanukuu maafisa wa utawala wa Biden ambao hawakutajwa majina.
Seneta wa Marekani Chris Coons alipongeza Baraza la Seneti kwa kupitisha kwa kauli moja azimio lake ambalo linalaani rekodi ya haki za binadamu ya serikali ya Eswatini na mauaji ya mwanaharakati wa haki za binadamu wa Eswatini Thulani Maseko.
Baraza la Seneti la Marekani limepiga kura ya kutupilia mbali vifungu vyote vya mashtaka dhidi ya waziri wa Usalama wa Ndani, Alejandro Mayorkas, na kumaliza kesi yake, kuhusiana na jinsi alivyoshughulikia mpaka wa Marekani na Mexico.
Moscow imekwepa kulaani shambulizi la Iran dhidi ya Israel wakati ikiwataka viongozi wa Israel kujizuia.
Waziri Mkuu wa Qatar na Waziri wa Mambo ya Nje, Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al thani amesema leo kuwa mashauriano kwa sitisho jipya la mapigano huko Gaza yako katika ‘awamu nyeti.’
Waziri wa Ulinzi wa Israel alisema Jumanne vitisho vya Iran havitazuia taifa lake kujibu mashambulizi ya anga ya Jumapili dhidi ya taifa hilo la Kiyahudi.
Mkutano wa ngazi ya juu wa kuahidi misaada kwa Ethiopia, uliofadhiliwa na Ethiopia, Uingereza, na Umoja wa Mataifa ulipokea karibu dola milioni 628.9 kama msaada wa kibinadamu wa kuokoa maisha kwa mamilioni ya raia wa nchi hiyo wanaoteseka.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema Jumatatu kwamba wafadhili wa dunia wameahidi dola bilioni 2.1 kusaidia kukabiliana na mgogoro wa kibinadamu nchini Sudan, iliyoharibiwa na vita.
Wizara ya biashara ya Marekani Jumatatu imetoa mkopo wa dola bilioni 6.4 kwa kampuni ya elektroniki ya Samsung yenye makao yake Korea Kusini, ili kujenga kiwanda chake kipya cha kutengeneza chip za komputa mjini Taylor, Texas pamoja na kupanua kiwanda cha zamani mjini Austin kwenye jimbo hilo hilo.
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amesema Jumatatu kwamba taifa lake litatoa msaada wa kibinadamu wa euro milioni 244 zaidi kwa Sudan, taifa lililokumbwa na vita.
Kesi ya kwanza ya uhalifu inayomkabili Rais wa zamani wa Marekani inatarajiwa kuanza wiki hii huko New York.
Mashirika makubwa ya ndege katika eneo la Mashariki ya Kati yalitangaza kuwa yanaanza tena safari zao katika eneo hilo baada ya kuziahirisha au kubadilisha baadhi, wakati Iran iliporusha dazani za ndege zisizo na rubani na makombora dhidi ya Israel.
Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema leo kwamba Beijing ilipinga vikali “ udanganyifu wa siasa za umoja’ za Marekani, Japan, na Ufilipino na kukataa matamshi yaliyotolewa na waziri mkuu wa Japan Fumio Kishida na Rais wa Marekani Joe Biden kuhusu hatua za China kwenye South China Sea.
Russia katika siku za karibuni imefanya mashambulizi makubwa ya anga na ndege zisizokuwa na rubani kwa raia wa Ukraine na miundo mbinu ya nishati na kusababisha vifo na uharibifu mkubwa.
Wafanyakazi wa misaada nchini Sudan wamesema kwamba mapigano ya mwaka mmoja nchini humo yamesababisha mamilioni ya watu kukoseshwa makazi na kukabiliwa na njaa.
Kuongezeka kwa imani kwa wafuasi wa kundi la kigaidi la Islamic state kulikodhihirika katika mfululizo wa vitisho vya mtandaoni dhidi ya bara la Ulaya pamoja na shambulio baya la kundi hilo kwenye jumba la tamasha nchini Russia, kunawatia wasiwasi maafisa wa usalama wa Marekani.
Marekani na Japan Jumatano zilisherekea muungano wao wa miongo kadhaa, wakati Rais Joe Biden akimkaribisha White House waziri mkuu Fumio Kishida kwa ziara rasmi na chakula cha jioni.
Israel Jumatano iliwaua watoto watatu wa kiongozi mkuu wa Hamas Ismail Haniyeh katika shambulio la anga huko Gaza, ikisema ndugu hao walikuwa wanachama wa tawi la kijeshi la Hamas.
Pandisha zaidi