Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 02, 2024 Local time: 23:03

Samsung kujenga kiwanda kipya cha kutengeneza Chip za kompyuta Marekani


Afisaa wa ngazi ya juu wa Samsung akionyesha teknolojia za kampuni hiyo kwenye maonyesho mjini Las Vegas, Nevada. Januari 8, 2024.
Afisaa wa ngazi ya juu wa Samsung akionyesha teknolojia za kampuni hiyo kwenye maonyesho mjini Las Vegas, Nevada. Januari 8, 2024.

Wizara ya biashara ya Marekani Jumatatu imetoa mkopo wa dola bilioni 6.4 kwa kampuni ya elektroniki ya Samsung yenye makao yake Korea Kusini, ili kujenga kiwanda chake kipya cha kutengeneza chip za komputa mjini Taylor, Texas pamoja na kupanua kiwanda cha zamani mjini Austin kwenye jimbo hilo hilo.

Kupitia taarifa kutoka White House, Rais wa Marekani Joe Biden amesema kuwa mkopo huo ni sehemu ya mpango wa sheria ya 2022 CHIPS na Sayansi uliopitishwa na bunge, na ambao utasaidia Samsung kuongeza uwekezaji wake jimboni Texas hadi zaidi ya dola milioni 40 pamoja na kutoa zaidi ya ajira 20,000.

Biden ameongeza kusema kupitia taarifa kwamba viwanda hivyo vitatengeneza moja wapo ya chip zenye nguvu zaidi ulimwenguni, ambazo ni muhimu kwa teknolojia kama za AI, wakati pia zikiimarisha usalama wa taifa. Wizara ya biashara imesema kwamba kiwanda kipya cha Samsung mjini Tylor kitajumuisha utafiti na maendeleo pamoja na sehemu ya kisasa ya kupakia, kabla ya kutumika kwenye mifumo ya elektroniki.

Forum

XS
SM
MD
LG