Manyanyaso ya kingono, ghasia za kikabila, na kuharibiwa kwa miundo mbinu pia zimeripotiwa, wakati ulimwengu ukionekana kuangalia kando. Taifa hilo la kaskazini mashariki mwa Afrika linashuhudia moja ya majanga mabaya zaidi ya kibinadamu katika siku za karibuni, pamoja na idadi kubwa sana ya watu waliokoseshwa makazi duniani, kulingana na Umoja wa Mataifa.
Taifa hilo pia linaelekea kutumbukia kwenye janga kubwa sana la baa la njaa, taarifa zimeongeza. Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, wafanyakazi wa misaada wameliita janga hilo kuwa “vita vilivyosahauliwa,” linalowaathiri watu milioni 48 katika nchi hiyo, ambapo zaidi ya nusu wanahitaji misaada ya kibinadamu.
Wataalam wanasema kwamba hakuna dalili ya kumalizika kwa mapigano hayo yaliyoanza Aprili 15 mwaka uliopita, kati ya mkuu wa jeshi Abdel Fattah al–Burhan, na aliyekuwa naibu wake Mohamed Hamdan Dagalo, ambaye anaongoza kundi la kijeshi lenye silaha la Rapid Support Forces, au RSF.
Forum