Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 07:31

China yapinga vikali 'udanganyifu wa siasa za umoja ' za Marekani, Japan na Ufilipino


Rais Joe Biden akutana na Waziri Mkuu wa Japan Kishida na Rais wa Ufilipino Marcos Jr. mjini Washington
Rais Joe Biden akutana na Waziri Mkuu wa Japan Kishida na Rais wa Ufilipino Marcos Jr. mjini Washington

Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema Ijumaa Beijing ilipinga vikali “ udanganyifu wa siasa za umoja" za Marekani, Japan, na Ufilipino.

Rais wa China Xi Jinping
Rais wa China Xi Jinping

China pia imepinga matamshi yaliyotolewa na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida na Rais wa Marekani Joe Biden kuhusu hatua za China kwenye eneo la South China Sea.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa China Mao Ning amesema Ijumaa kwamba taarifa iliyotolewa na nchi hizo tatu kuhusu hatua za China katika South China Sea ambapo walielezea kuwa ni za “ hatari na uchokozi”zimebadilika kutoka kwenye ukweli wa kimsingi.

Rais Joe Biden alimpokea Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida na Rais wa Ufilipino Ferdinand Marcos Jr, siku ya Alhamisi akilenga kutuma ujumbe wa wazi kwa Beijing kwamba ni lazima isitishe tabia zake za uchokozi dhidi ya majirani zake wa South China Sea.

Rais wa Marekani alisisitiza kwamba shambulizi lolote kwa Ufilipino litapelekea mkataba wa pamoja wa ulinzi baina ya Washington na Manila.

Ferdinand Marcos jr, rais wa Philippine alikuwa na haya ya kusema:

“kukabiliana na changamoto za wakati wetu kunahitaji juhudi za pamoja kwa upande wa kila mtu, kujitolea kwa madhumuni ya pamoja na nia ya dhati ya kutoyumba yumba kwa utaratibu wa kimataifa unaozingatia sheria.”

Forum

XS
SM
MD
LG