Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 20, 2024 Local time: 09:19

Zambia yafikia makubaliano muhimu ya kurekebisha deni lake la mabilioni ya dola


Rais wa Zambia Hakainde Hichilema akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa Ufaransa. Picha na Geoffroy VAN DER HASSELT / AFP.
Rais wa Zambia Hakainde Hichilema akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa Ufaransa. Picha na Geoffroy VAN DER HASSELT / AFP.

Zambia Jumatatu ilitangaza kwamba imeingia makubaliano ya kihistoria na wakopeshaji binafsi wanaomiliki Eurobond zenye thamani ya dola bilioni 3.5, na kuondoa kikwazo kikubwa katika marekebisho ya muda mrefu ya deni la nchi hiyo.

“Historia imeandikwa. Tunayofuraha kutangaza makubaliano na wamiliki wa Eurobond”, Rais Hakainde Hichilema alisema kwenye mtandao wa X.

“Hii ni kurekebisha deni la zaidi ya dola bilioni 3.5 chini ya mfumo wa pamoja wa G20,” aliongeza.

Zambia, mzalishaji mkubwa wa shaba barani Afrika, ilishindwa kulipa deni lake la nje la dola bilioni 18.6 mwaka wa 2020 lakini mazungumzo yalikwama juu ya tofauti kati ya China na wakopeshaji wa nchi za Magharibi.

Hichilema alisema mwezi Disemba kwamba asilimia 98 ya wakopeshaji rasmi sasa wamesaini makubaliano ya awali ya kurekebisha deni la Zambia ambalo lilikadiriwa kufikia dola bilioni 32.8 mwaka 2022.

Forum

XS
SM
MD
LG