Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 17, 2024 Local time: 14:01

Marekani na Japan kuimarisha ushirikiano kwenye sekta ya teknolojia na ulinzi


Rais wa Marekani Joe Biden na waziri mkuu wa Japan Fumio Kishida wakifanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari, White House, Aprili 10, 2024. Picha ya AFP
Rais wa Marekani Joe Biden na waziri mkuu wa Japan Fumio Kishida wakifanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari, White House, Aprili 10, 2024. Picha ya AFP

Marekani na Japan Jumatano zilisherekea muungano wao wa miongo kadhaa, wakati Rais Joe Biden akimkaribisha White House waziri mkuu Fumio Kishida kwa ziara rasmi na chakula cha jioni.

Viongozi hao walitangaza mipango mipya kuhusu sekta ya teknolojia na ulinzi, ikiwemo kuboresha makubaliano ya kamandi na udhibiti kwa jeshi la Marekani na Japan, uwekezaji mpya na ushirikiano kwenye sekta ya anga, ujasusi bandia, vifaa vya kusambaza nguvu ya umeme na nishati safi.

Lakini lengo kuu ni kuzuia mashambulizi ya kijeshi ili kuimarisha ushirikiano wa baharini katika bahari ya Kusini mwa China, pamoja na ulinzi wa anga.

“Kwa mara ya kwanza, Japan na Marekani na Australia zitaunda mfumo wa mtandao wa makombora ya anga na ulinzi,” Biden alisema.

Forum

XS
SM
MD
LG