Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 08, 2024 Local time: 20:43

China yataka sitisho la vita baina ya Russia na Ukraine


Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Lavrov akutana na Rais wa China Xi Jinping mjini Beijing.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Lavrov akutana na Rais wa China Xi Jinping mjini Beijing.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi alitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano haraka iwezekanavyo nchini Ukraine.

Hatua hii imekuja baada ya kuzungumza na mwenzake wa Russia mjini Beijing. Alisema China inalenga kuona vita vimesitishwa na kumalizika hivi karibuni.

Katika mkutano na Rais Xi Jinping wa China Jumanne, Lavarov alisema kuchaguliwa tena kwa Vladimir Putin kama Rais wa Russia kumehakikisha maendeleo zaidi ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Rais Xi Jinping, kushoto,alipokutana na Rais wa Russia Vladimir Putin Kremlin, Moscow, Russia Machi 20, 2023.
Rais Xi Jinping, kushoto,alipokutana na Rais wa Russia Vladimir Putin Kremlin, Moscow, Russia Machi 20, 2023.

Alishutumu "vikwazo visivyo halali" vilivyowekwa na Magharibi dhidi ya Russia na nchi nyingine.

Lavrov aliwasili Beijing Jumatatu ili kuonyesha ushirikiano na mshirika wa karibu wa kidiplomasia China. huku kukiwa na vita vikali vya Moscow dhidi ya Ukraine na juhudi zinazoendelea za kuoanisha sera zao za kigeni dhidi ya Marekani na washirika wake.

Forum

XS
SM
MD
LG