Marekani Jumanne ililishinikiza kundi la Hamas kukubali makubaliano ya kusitisha mapigano na Israel huko Gaza kwa muda wa wiki sita, na pia kuachiliwa huru kwa mateka 100 wanaoshikiliwa na kundi hilo, ili Israel nayo iwaachilie huru mamia ya Wapalestina iliowafunga jela.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, alisema Jumatatu kwamba tarehe ya mashambulizi ya ardhini, yakilenga mji wa kusini mwa Gaza wa Rafah, imepangwa, lakini bila kutaja ni lini.
Wakazi wa Marekani wanajiandaa kushuhudia tukio kubwa la kupatwa kwa jua Aprili Nane.
Katika mahojiano na VOA, kampeni ya Rais Joe Biden ya kutaka kuchaguliwa tena haikutilia maanani tukio moja la rekodi ya uchangishaji fedha lililofanyika Jumamosi na kampeni ya Donald Trump.
Jeshi la Israel limesema Jumatatu kwamba limefanya shambulizi la anga kusini mwa Lebanon, ambalo limeua kamanda mmoja wa kundi la Hezbollah aliyeongoza mashambulizi kadhaa yakilenga kaskazini mwa Israel.
Joe Biden na Donald Trump wameshinda uchaguzi wa awali katika vyama vyao kwenye jimbo la Magharibi kati la Wisconsin wiki hii, huku wote wakiwa na uhakika wa uteuzi.
Israel itaruhusu uwasilishaji wa "muda" wa misaada kupitia mpaka wake na Ukanda wa kaskazini wa Gaza, ofisi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ilitangaza siku ya Ijumaa.
Senegal itafanya ukaguzi wa sekta za mafuta, gesi na madini, rais mteule wa Senegal Bassirou Diomaye Faye alisema Jumatano katika hotuba kwa taifa kwa njia ya televisheni, huku akiwahakikishia wawekezaji kwamba wamekaribishwa nchini.
Kundi la Misaada la World Central Kitchen, WCK, limesema Jumanne kwamba shambulizi la anga la Israel limeuwa wafanyakazi wake 7 huko Gaza, na hivyo linasitisha mara moja shughuli zake katika eneo hilo.
Wanajeshi wa Afrika Kusini waliopelekwa DRC kusaidia kuleta utulivu wanasema baadhi yao hawana silaha, na wanatarajiwa kupambana na waasi wa M23 bila msaada wa helikopta za usafiri.
Maafisa wa Taliban kusini mashariki mwa Afghanistan walisema Jumatatu bomu la kutegwa ardhini lililipuka usiku na kuua watoto wasiopungua tisa.
Kundi la mamluki la Russia la Wagner, linalisaidia wanajeshi wa serikali ya Mali wakati wa mashambulizi ya ndege zisizo na rubani katikati na kaskazini mwa nchi na kusababisha vifo vya raia kadhaa wengi wakiwa ni watoto.
Barack Obama, Bill Clinton pamoja na watu wenye majina makubwa kwenye tasnia ya burudani waliungana pamoja huko New York Alhamisi usiku kumkaribisha rais Joe Biden ambaye amechangisha kiwango kikubwa cha fedha dola milioni 26 kwa kampeni yake ya kuchaguliwa.
Mahakama ya juu ya Umoja wa mataifa Alhamisi iliamuru Israel kufungua njia zaidi za ardhini kuelekea Gaza ili kuruhusu misaada zaidi ya kibinadamu kwa Wapalestina wenye njaa kuingia kwenye eneo hilo.
Israel Jumatano ilikubali kutuma wapanga mikakati wake wa vita Washington kujadili nia yake ya kuanzisha mashambulizi ya ardhini dhidi ya wanamgambo wa Hamas katika mji wa kusini mwa Gaza wa Rafah.
Russia ilisema Jumatano imezuia mashambulizi ya roketi yaliofanywa na Ukraine yakiulenga mkoa wa Belgorod, wakati Ukraine ilisema Russia imeishambulia usiku kucha kwa droni 13.
Makamu wa rais mteule wa Taiwan Hsiao Bi-Khim amekamilisha ziara yake ya kidiplomasia ya Ulaya wiki iliyopita, suala ambalo limekera Beijing, wakati akisimama kwenye mataifa matatu pamoja na kukutana na wanasiasa kadhaa mjini Brussels.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema Jumatano kwamba haiungi mkono mpango wa Pakistan kujenga bomba la kusafirisha gesi kutoka Iran. Msemaji wa wizara hiyo Mathew Miller hata hivyo alikataa kutoa taarifa za kina kuhusu suala hilo.
Wanamgambo wa Hezbollah wa Lebanon, Jumatano wamefanya mashambulizi ya roketi kaskazini mwa Isreal, wakijibu mashambulizi ya anga ya Israel yaliyouwa watu 7 kusini mwa Lebanon.
Watoto wengi sana nchini Haiti wako katika hatari ya kifo huku magenge yakiimarisha nguvu zao na mzozo wa kibinadamu ukiwa mbaya zaidi, mkurugenzi wa shirika la Umoja wa mataifa linalohudumia watoto (UNICEF) Catherine Russell alisema Jumanne.
Pandisha zaidi