Taarifa kutoka jeshi hilo imemtambulisha kamanda huyo kama Ali Ahmad Hassin, kutoka kikosi cha Hezbollah cha Radwan. Kundi hilo la wapiganaji pia limetangaza kifo cha mpiganaji wake kwa jina hilo hilo, bila kutoa maelezo zaidi. Taarifa kutoka kwa jeshi la Israel zimeongeza kuwa shambulizi hilo pia limeua watu wengine wawili.
Mashambulizi ya mpakani kati ya vikosi vya Israel na wapiganaji wa Hezbollah yamekuwa jambo la kawaida kwa miezi 6 sasa, tangu kuzuka kwa vita kati ya Israel na kundi la Hamas linaloungwa mkono na Hezbollah, huko Ukanda wa Gaza. Kwenye taarifa tofauti, jeshi la Isreal limesema kwamba limefanya mashambulizi ya anga huko Khan Younis kusini mwa Gaza, yakiwa majibu kutokana na mashambulizi kadhaa ya roketi kutoka Hamas.
Maafisa wa Israel Jumapili walitangaza kuondolea vikosi vyake kutoka Khan Younis. Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant amesema kuwa vikosi hivyo vimeondolewa wakati vikijitayarisha kuanza operesheni nyingine, inayojumuisha kuingia mji wa Rafah.
Forum