Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 23:29

Marekani yaonya Pakistan dhidi ya bomba la gesi kutoka Iran


Wafanyakazi wa Iran wakiendelea na ujenzi wa bomba la gesi kuelekea Pakistan karibu na mpaka wa Chabahar, Machi 11, 2013.
Wafanyakazi wa Iran wakiendelea na ujenzi wa bomba la gesi kuelekea Pakistan karibu na mpaka wa Chabahar, Machi 11, 2013.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema Jumatano kwamba haiungi mkono mpango wa Pakistan kujenga  bomba la kusafirisha gesi kutoka Iran. Msemaji wa wizara hiyo Mathew Miller hata hivyo alikataa kutoa taarifa za kina kuhusu suala hilo.

Hata hivyo, aliitahadharisha Islamabad dhidi ya kusonga mbele na mpango huo. “Siku zote tunamshauri yeyote anayetaka kufanya biashara na Iran, kuwa kuna hatari ya kuwekewa vikwazo vyetu, na tungemshauri kila mmoja kufikiria hilo kwa makini sana,” amesema Miller, akiongeza kuwa naibu waziri wa mambo ya nje aliweka bayana wiki iliopita kuwa Marekani haiungi mkono mradi huo kusonga mbele.

Donald Lu, waziri mdogo wa mambo ya nje kwa Asia kusini na Kati aliiambia kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge Jumatano iliyopita kwamba, uagizaji wa gesi kutoka Iran ungepelekea Pakistan kuwekewa vikwazo na Marekani. Serikali ya muda ya Pakistan inayoondoka mamlakani imeidhinisha ujenzi wa bomba la mafuta lenye urefu wa kilomita 80 mwezi uliopita, kwa sehemu kubwa ikionkena kama kukwepa kuilipa Iran dola bilioni 18 kama faini ya kuchelewesha mradi huo kwa miaka kadhaa.

Matamshi ya Miller yamekuja wakati vyombo vya habari vya Pakistan vikiripoti Jumanne kwamba Islamabad inapanga kuomba kuepushwa na vikwazo vya Marekani.

Forum

XS
SM
MD
LG