Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 10, 2024 Local time: 23:14

Bomu la kutegwa ardhini lalipuka na kuua watoto wasiopungua tisa


FILE - Picha hii imechukuliwa Nov. 9, 2021 ikionyesha mmoja wa wafanyakazi wa Taasisi ya HALO Trust ikitumia chombo cha kutafuta mabomu yaliyotegwa ardhini katika kijiji cha Nad-e-Ali huko jimbo la Helmand.
FILE - Picha hii imechukuliwa Nov. 9, 2021 ikionyesha mmoja wa wafanyakazi wa Taasisi ya HALO Trust ikitumia chombo cha kutafuta mabomu yaliyotegwa ardhini katika kijiji cha Nad-e-Ali huko jimbo la Helmand.

Maafisa wa Taliban kusini mashariki mwa Afghanistan walisema Jumatatu bomu la kutegwa ardhini lililipuka usiku na kuua watoto wasiopungua tisa.

“Bomu lililokuwa halijalipuka” lilikuwa ni mabaki ya mizozo ya zamani, lililipuka Jumapili wakati kikundi cha watoto wa kiume na wakike wakilichezea katika wilaya ya Geru, huko jimbo la Ghazni, alisema msemaji wa serikali ya jimbo.

Hamidullah Nisar alidai kuwa bomu hilo liliachwa wakati wa uvamizi wa Russia nchini Afghanistan katika miaka ya 1980.

Umoja wa Mataifa mjini Kabul ulisema Jumatatu kuwa maelfu ya raia, wakiwemo wanawake na watoto, nchini Afghanistan waliuawa au kujeruhiwa na mabomu ya kutegwa ardhini na vilipuzi vingine vilivyobakia baada ya vita.

Ilibandika katika mtandao wa X, ambao awali ulijulikana kama Twitter, kuwa UN “Washirika wa MinAction walikuwa wameondoa mabomu eneo la kilomita 3,011 (1,162 mi2),” wakisisitiza kuwa “kazi zaidi” inahitajika kuwalinda Waafghanistan, ikitokana na miongo kadhaa ya migogoro.

Afghanistan imepitia miaka kadhaa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe miaka ya 1990 baada ya majeshi ya Russia kuondoka nchini, na kumaliza kipindi cha muongo mmoja wa uingiliaji kati wa kijeshi nchini humo.

Wataliban wenye misimamo mikali waliibuka washindi katika mapambano ya kuchukua madaraka kati ya vikundi mbalimbali vya Afghanistan, wakichukua udhibiti wa sehemu kubwa ya nchi hiyo mwaka 1996 na kuitawala kwa kutumia tafsiri yenye msimamo mkali ya sheria za Kiislam.

Watawala wenye msimamo mkali waliondolewa madarakani miaka mitano baadae wakati Marekani na washirika wake walipoivamia Afghanistan kuwaadhibu wale waliokuwa wanawahifadhi al-Qaida waliopanga shambulizi la kigaidi la Septemba 2001 katika miji ya Marekani.

Forum

XS
SM
MD
LG