Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 09, 2024 Local time: 12:44

Pakistan imefanya mashambulizi ya anga kwa wanamgambo wa Afghanistan


Mfano wa wanamgambo wa TTP
Mfano wa wanamgambo wa TTP

Mashambulizi yalilenga makamanda wenye uhusiano na Tehrik-e-Taliban Pakistan au TTP.

Pakistan ilifanya mashambulizi ya anga ya mpakani dhidi ya maficho ya washukiwa wanamgambo nchini Afghanistan mapema Jumatatu, na kuua watu kadhaa, kwa mujibu wa maafisa.

Afisa wa usalama wa Pakistan, akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina na VOA kwa sababu hana mamlaka ya kuzungumza na vyombo vya habari, alithibitisha mashambulizi hayo ya awali, akisema yalilenga makamanda wenye uhusiano na Tehrik-e-Taliban Pakistan au TTP, taasisi ya kigaidi iliyoteuliwa kimataifa kufanya kazi nje ya nchi jirani.

Hatua hiyo ya kijeshi inaonekana ni kulipiza kisasi kwa uvamizi wa Jumamosi wa TTP dhidi ya kambi ya kijeshi ya Pakistan katika wilaya tete ya mpakani ya North Waziristan, ambalo liliwaua wanajeshi saba, wakiwemo maafisa wawili.

Serikali ya Taliban nchini Afghanistan imethibitisha katika taarifa yake kwamba ndege za Pakistan zilishambulia maeneo kadhaa katika majimbo yake ya kusini mashariki ya Paktika na Khost lakini ilidai kuwa shambulio hilo lilisababisha vifo vya raia wanane, wakiwemo wanawake na watoto.

Haikuwezekana kuthibitisha utambulisho wa watu waliouawa kutoka vyanzo huru.

Forum

XS
SM
MD
LG