Serekali ya Taliban, imesema waathirika walikuwa wamekusanyika nje ya benki inayoendeshwa rasmi ya New Kabul, kupokea mishahara yao wakati mjitoa muhanga alipotegua vilipuzi alivyovifunga mwilini mwake.
Walioshuhudia na maafisa wa eneo wameripoti kwamba walio jeruhiwa walipelekwa kwenye hospitali ya eneo hilo wengine wakiwa wamepata majeraha mabaya.
Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Taliban, katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, amesema shambulizi hilo linafanyiwa uchunguzi. Hakuna kundi ambalo limetangaza kuhusika na shambulizi hilo baya.
Forum