Rais wa Marekani Joe Biden Jumanne ameeleza kubomoka kwa daraja la Baltimore ni “ajali mbaya,” na kuahidi kurejesha huduma za bandari kuu ya East Coast kwa haraka iwezekanavyo baada ya meli ya mizigo kugonga nguzo ya daraja hilo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akutana na Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant Jumatatu katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani mjini Washington.
Kuongezeka kwa ghasia nchini Mali, Burkina Faso na Niger, kumewalazimisha takriban watoto milioni 1.8, kuhama makazi yao, likiwa ongezeko mara tano, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, shirika la hisani Save the Children, lilisema Alhamisi.
Moshi mkubwa umetanda katika anga ya ukanda wa gaza leo wakati Israel ikiendelea na mashambulizi.
Uingereza Jumatano imetangaza upelekaji mpya wa chakula huko Ukanda wa Gaza, wakati maafisa wa Marekani wakishinikiza kuongezwa kwa misaada ya kibinadamu, pamoja na sitisho jipya la mapigano, kabla ya mazungumzo na maafisa wa Israel mjini Washington, wiki ijayo.
Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi, Jumatano amekutana na mwenzake wa Australia Penny Wong mjini Canberra, ikiwa ni dalili ya kuimarika kwa uhusiano ya mataifa hayo jirani, kwenye eneo la Asia Pacific.
Vikwazo vya kimataifa vimechangia kuzorota kwa haki za binadamu nchini Korea Kaskazini, kwa mujibu wa shirika lisilo la kiserikali la Human Rights Watch, huku Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, ambayo inaunga mkono vikwazo hivyo, ikisema utawala wa nchi hiyo, ndio wa kulaumiwa zaidi, kwa hali hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema mwaka 2024 ni mwaka wa uchaguzi usio wa kawaida wa kuangazia hatari kwa habari potofu na za uongo katika mitandao kwenye Mkutano wa demekrasia unaofanyika mjini Seoul leo.
Mashirika kadhaa ya serikali na yale ya kutoa misaada nchini Haiti yameripoti kuwa vifaa vyao, pamoja na misaada imeporwa, huku nchi hiyo ikiingia kwenye wimbi jingine la ghasia za magenge.
Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu alisema Jumapili kwamba wanajeshi wa Israel wataendesha mashambulizi ya ardhini yaliyopangwa katika mji wa kusini wa Rafah, katika ukanda wa Gaza, ambayo yamezua hofu ya uwezekano wa mauaji makubwa ya raia.
US SCHUMER-ISRAEL Kiongozi wa walio wengi katika Baraza la Seneti la Marekani Chuck Schumer, ambaye ni afisa wa ngazi ya juu Myahudi nchini Marekani, Alhamisi alitoa wito kwa Israel kuitisha uchaguzi mpya.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken Jumatano alisema kwamba Israel yapaswa kuzingatia usalama wa raia wa Palestina kama kipaumbele cha kwanza katika vita vyake dhidi ya Hamas huko Gaza.
Rais wa Marekani Joe Biden Jumanne aliwapokea kwenye White House Rais wa Poland Andrzej Duda na waziri mkuu Donald Tusk, huku kukiwa wasiwasi juu ya ufadhili wa baadaye wa Marekani kuisaidia Ukraine kujihami dhidi ya uvamizi wa Russia.
Meli ya misaada kutoka Uhispania iliyobeba tani 200 za msaada wa chakula ilisafiri kutoka Cyprus hadi huko Gaza Jumanne, zikiwa juhudi za hivi karibuni za kugawa chakula kwa maelfu ya Wapalestina wanaokabiliwa na njaa, huku mapigano kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas yakizidi kupamba moto.
Waislamu katika nchi nyingi ulimwenguni wameanza mwezi mtukufu wa Ramadhani wakati nchi kadhaa za Afrika zitaanza kufunga Jumanne, huku wakitafakari hali ngumu inayowakumba Waislamu Wapalestina huko Gaza.
Wakati wapiga kura wa Marekani wanajitayarisha kwa duru nyingine ya chaguzi za awali siku ya Jumanne, Rais wa Marekani, Joe Biden na mpinzani wake wa kisiasa Mrepublican Donald Trump walisafiri mwishoni mwa wiki kwenda kwenye majimbo ambayo matokeo yanaweza kwenda upande wowote.
Tawi la Al-Qaida nchini Yemen Jumatatu limetangaza kifo cha kiongozi wake Khalid al Batarfi kilichotokea Jumapili.
Wakati wapalestina wameanza mwezi mtukufu wa Ramadan, Israel imetangaza mapema Jumatatu, kuwa imefanya mashambulizi kote kwenye Ukanda wa Gaza.
Shirika moja la hisani la Marekani limesema kwamba linapakia misaada kuelekea Gaza kwenye meli moja nchini Cyprus, ukiwa msaada wa kwanza kupitia kwenye njia ya bahari, kwelekea eneo lililokumbwa na vita, ambayo Tume ya Umoja wa Mataifa inatumai itafunguliwa wikiendi hii.
Milio ya risasi imesikika usiku wa kuamkia Jumamosi kwenye mji mkuu wa Haiti wa Port-au-Prince, mwanahabari wa AFP alieko huko amesema, huku wakazi wakiendelea kutafuta hifadhi, kufuatia kuzuka kwa ghasia za magenge siku chache zilizopita chini humo.
Pandisha zaidi