Mfalme wa Saudi Arabia Salman bin Abdulaziz ametumia kuanza kwa mwezi wa Ramadhani kutoa wito wa kukomeshwa uhalifu mbaya sana unaofanyika katika Gaza iliyokumbwa na vita.
Akizungumza kama msimamizi wa maeneo mawili matakatifu ya Kiislamu mfalme wa Saudi Arabia ametoa ujumbe wa shukrani wa ramadhani Jumapili jioni kwa Baraka ulizopewa ufalme wa Saudi arabia lakini alibainisha kuwa vita vya Gaza vitafunika mwezi wa ramadhani wa kufunga na kuomba .
Waislamu kote ulimwenguni wanasema kwamba mwaka huu utakuwa mgumu kwao kutokana na kiwango kikubwa cha mfumuko wa bei na gharama kubwa ya chakula kikuu kinacholiwa kipindi cha Ramadhan.
Wakati wa Ramadhani waislamu wanafunga kula na kunywa na kitamaduni wanakutana majira ya jioni na familia na marafiki kufungulia na wanaamini kwamba kufunga kunasafisha mwili na wakati huu inawakumbusha mateso wanayopitia masikini.
Baadhi ya taarifa za habari hii zinatokana na vyanzo mbalimbali vya habari.
Forum