Ghasia hizo zimeendelea hata baada ya wiki kadhaa za mashauriano yaliyoijumuisha Misri, Marekani na Qatar, yakijaribu kupatikana kwa sitisho la mapigano, kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hamas, kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadan, ambayo yangehusisha kuachiliwa kwa mateka wanaoendelea kushikiliwa na Hamas huko Gaza, pamoja na kuachiliwa kwa wafungwa wa Palestina wanaoshikiliwa na Israel.
Wapatanishi wa Hamas kwenye mazungumzo hayo wakati wakiondoka mjini Cairo wiki iliyopita, walisema kwamba mazungumzo hayo yataanza tena wiki hii. Jeshi la Israel limesema kwamba operesheni zake zimehusisha mashambulizi ya anga pamoja na ya ardhini mjini Khan Younis, na maeneo mengine kusini na kati kati mwa Gaza. Wizara ya afya ya Gaza imesema Jumatatu kwamba watu 67 wameuliwa kwenye mashambulizi ya Israel katika siku moja iliyopita, wakati jumla ya watu 31,112 wakiwa wamekufa tangu mapigano yalipozuka Oktoba.
Forum