Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 09, 2024 Local time: 02:03

Meli ya jeshi la Marekani inaelekea Mediterranean kutoa misaada kwa Gaza


Misaada zaidi ya kibinadamu inahitajika huko Gaza kufuatia mapigano kati ya Israel na Hamas. Jan. 24, 2024.
Misaada zaidi ya kibinadamu inahitajika huko Gaza kufuatia mapigano kati ya Israel na Hamas. Jan. 24, 2024.

Israel imesema inakaribisha usafirishaji wa baharini na huenda itakagua mizigo inayoelekea Gaza

Meli ya jeshi la Marekani iliyobeba vifaa kwa ajili ya ujenzi wa gati ya muda huko Gaza iko njiani kuelekea Mediterranea siku ya Jumapili ikiwa ni siku tatu baada ya Rais wa Marekani Joe Biden kutangaza mipango ya kuongeza upelekaji wa misaada kwa njia ya bahari hadi kwenye eneo lililozingirwa ambako maelfu ya Wa-palestina wamekuwa wakikabiliwa na njaa.

Kufunguliwa njia hiyo ya bahari, pamoja na kudondosha misaada kwa njia ya anga kunakofanywa na Marekani, Jordan na wengine kulionyesha kuongezeka kwa mgogoro wa kibinadamu huko Gaza, na azma mpya ya kuachana na udhibiti wa Israeli juu ya usafirishaji kwa njia ya ardhi.

Israel imesema inakaribisha usafirishaji wa baharini na huenda itakagua mizigo inayoelekea Gaza kabla ya kuondoka katika eneo karibu na Cyprus. Idadi ya kila siku ya malori ya misaada yanayoingia Gaza kwa njia ya ardhi katika kipindi cha miezi mitano iliyopita imekuwa chini ya 500 ambayo iliingia kabla ya vita kwa sababu ya vizuizi vya Israeli na masuala ya usalama.

Forum

XS
SM
MD
LG