Chakula hicho ambacho kilikusanywa na World Central Kitchen, shirika la hisani lililoanzishwa na mpishi mashuhuri Jose Andres, kilikuwa kwenye meli kikivutwa na meli ya kundi la misaada la Uhispania la Open arms na kuelekea eneo ambalo halikutajwa kwenye pwani ya Gaza. Safari hiyo ya kilomita 400 inatarajiwa kuchukua siku mbili hadi tatu.
Meli ya pili ilikuwa ikipakiwa nchini Cyprus ili kufanya safari hama hiyo siku za karibuni kusaidia Wapalestina waliozingirwa, waziri wa mambo ya nje wa Cyprus Constantinos Kombos aliiambia radio ya serikali. Akizungumza baadaye mjini Beirut, Kombos alisema, “Tunafanya kazi ili shehena ya kwanza ifike salama na kisha kuwepo usambazaji salama.”
“Ikiwa yote yatafanyika kama tulivyopanga, tayari tumeweka utaratibu wa kupeleka shehena ya pili na kubwa zaidi, na tutafanya kazi ili zoezi hili lifanyike kila mara kwa kuongeza misaada mingi zaidi,” alisema.
“Tunaweza kuleta mamilioni ya chakula kwa siku,”, Andres alisema. “Wakazi wa Gaza watapewa chakula,” aliongeza.
Forum