Meli hiyo yenye bendera ya Uhispania kwa jina Open Arms, ilitia nanga wiki tatu zilizopita kwenye bandari ya Larnaca, Cyprus, ambayo ni nchi mwanachama wa EU inayokaribia zaidi Ukanda wa Gaza.
Wafanyakazi wa shirika hilo la misaada kwa jina World Central Kitchen wamekuwa wakipakia misaada ya kibinadamu kwenye boti hiyo tayari kuelekea Gaza, limesema kupitia taarifa. Akiwa kwenye mji wa Larnaca, mkuu wa EU Ursula von der Leyen awali alieleza matumaini yake kwamba njia hiyo ya bahari ingefunguliwa leo Jumamosi, bila kutoa maelezo zaidi.
Sasa hivi hakuna bandari zinazofanya kazi huko Gaza, na haijaelezwa ni wapi boti hiyo itakaposhusha mizigo yake, watakaoisambaza, na iwapo itakaguliwa na Israel. Pentagon Ijumaa imesema kwamba Marekani inapanga kujenga bandari ya muda kwenye ufukwe wa Gaza, ndani ya muda wa siku 60, ikihusisha zaidi ya wafanyakazi 6,000 kutoka Marekani.
Forum