Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 23:13

Netanyahu asisitiza Israeli itaendelea na operesheni ya Rafah licha ya jumuiya ya kimataifa kupinga


W3aziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu.
W3aziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu.

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu alisema Jumapili kwamba wanajeshi wa Israel wataendesha mashambulizi ya ardhini yaliyopangwa katika mji wa kusini wa Rafah, katika ukanda wa Gaza, ambayo yamezua hofu ya uwezekano wa mauaji makubwa ya raia.

"Hakuna shinikizo la kimataifa litakalotuzuia kufikia malengo yote ya vita, kuondoa Hamas, kuwaachilia mateka wetu wote na kuhakikisha kuwa Gaza haitakuwa tishio tena kwa Israeli," Netanyahu aliambia mkutano wa baraza la mawaziri katika video iliyotolewa na afisi yake.

"Ili kutimiza hayo, tutafanya pia operesheni huko Rafah," alisema.

Maoni yake yamekuja huku mazungumzo yakitarajiwa kuanza tena mjini Doha, Qatar, kutafuta makubaliano ya amani huko Gaza, ambapo Israel imeendeleza vita dhidi ya wanamgambo wa Hamas kwa zaidi ya miezi mitano.

Wajumbe wa baraza la mawaziri la Israel walipangwa kujadili "mamlaka" ya timu ya mazungumzo baadaye Jumapili, afisi ya Netanyahu imesema. Netanyahu alitarajiwa kukutana na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, ambaye alitarajiwa kusisitiza onyo lake dhidi ya mashambulizi ya ardhini ya Rafah.

Wengi wa watu milioni 2.4 wa Gaza wametafuta hifadhi kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara ya Israel katika mji huo wa kusini. Rais wa Marekani Joe Biden, ambaye ameiunga mkono Israel wakati wa vita, amesema uvamizi wa Rafah “haukubaliki" isipokuwa pawe na mipango madhubuti ya kulinda raia.

Forum

XS
SM
MD
LG