Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 16, 2024 Local time: 10:31

Vikwazo vimechangia kuzorota kwa haki za binadamu Korea Kaskazini - HRW


PICHA YA MAKTABA: Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.
PICHA YA MAKTABA: Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.

Vikwazo vya kimataifa vimechangia kuzorota kwa haki za binadamu nchini Korea Kaskazini, kwa mujibu wa shirika lisilo la kiserikali la Human Rights Watch, huku Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, ambayo inaunga mkono vikwazo hivyo, ikisema utawala wa nchi hiyo, ndio wa kulaumiwa zaidi, kwa hali hiyo.

Shirika hilo la kutetea haki za binadamu lilisema vikwazo vya Umoja wa Mataifa vilivyowekewa Korea Kaskazini mwaka wa 2016 na 2017 "vimevuruga biashara ya jumla ya mipakani" na China, na kupunguza uwezo wa watu kufanya shughuli zisizo rasmi za soko ili kuendeleza maisha yao.

Masoko yaliyoidhinishwa na serikali, na yale ya kibinafsi yamekuwa yakifanya kazi nchini Korea Kaskazini tangu mwishoni mwa miaka ya 1990, lakini vizuizi vikali vya nyakati za COVID-19 nchini humo viliwekwa mapema mwaka wa 2020, na kuifanya hali kuwa mbaya zaidi, ilisema Human Rights Watch (HRW) katika ripoti hiyo.

Marekani inasema utawala wa Korea Kaskazini ndio wa kulaumiwa kwa hali ilivyo nchini mwake.

Sauti ya Amerika ilijaribu kuufikia ujumbe wa Korea Kaskazini katika Umoja wa Mataifa kwa majibu ya ripoti ya HRW, pamoja na kauli iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Marekani, lakini haikupokea jibu.

Korea Kaskazini haijawaruhusu wafanyikazi wa kimataifa wa misaada kuingia nchini tangu walipoondoka zaidi ya miaka mitatu iliyopita.

Forum

XS
SM
MD
LG