Hospitali zimewarejesha nyumbani wagonjwa na kufuta upasuaji baada ya takriban theluthi mbili ya madaktari vijana nchini kugoma na kuondoka kazini wakipinga mpango wa serikali wa kuongeza udahili wa wanafunzi wanaosomea tiba vyuoni, ikizua hofu ya kuongezeka matatizo.
“Shughuli za taasisi za matibabu za umma zitaboreshwa kufikia upeo wake,” Waziri Mkuu Han Duck-soo aliuambia mkutano wa kusimamia majanga, akisema hospitali hizo zitakuwa wazi kwa muda mrefu na pia mwishoni mwa wiki na siku za sikukuu ili kukabiliana na ongezeko la wagonjwa.
Wakati mgomo huo ukiingia siku ya nne, wizara hiyo ya afya ilisema ilikuwa inaziruhusu hospitali mbalimbali na zahanati kutoa huduma za tiba kwa mitandao, kama vile ushauri na uandikishaji wa dawa ambao mpaka sasa unapatikana tu kwa ufinyu.
Zaidi ya madaktari walio katika mafunzo kazini 7,800 na walio katika majaribio wamegoma, wizara hiyo iliongeza.
Hiyo ni sehemu ndogo tu ya idadi ya madaktari 100,000 nchini, lakini wana majukumu muhimu katika shughuli za kila siku kwenye hospitali zinazotoa taaluma ya udaktari, ikiwa inaweza kufikia zaidi ya asilimia 40 ya wafanyakazi, huku uokoaji wa gharama ukiwafanya kivutio kwa mahospitali makubwa.
Wanafanya kazi muhimu katika vyumba vya dharura, kitengo cha wagonjwa mahututi na vyumba vya upasuaji katika hospitali kubwa zinazowatibu wagonjwa waliopewa rufaa kutoka hospitali ndogo na zahanati binafsi.
.
Forum