Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 28, 2025 Local time: 04:48

Mgomo wa madaktari waendelea Jumapili mjini Seoul


Madaktari wa Korea Kusini ambao wamekuwa kwenye mgomo wa wiki mbili mjini Seoul. Picha ya maktaba.
Madaktari wa Korea Kusini ambao wamekuwa kwenye mgomo wa wiki mbili mjini Seoul. Picha ya maktaba.

Maelfu ya madaktari waliohudumu kwa muda mrefu, Jumapili wameandamana mjini Seoul, Korea Kusini, ili kuonyesha uungaji mkono kwa wenzao chipukizi, ambao wamekuwa kwenye maandamano kwa karibu wiki mbili.

Madaktari hao wamekuwa wakilalamikia mpango wa serikali wa kuongeza kwa kiwango kikubwa ada ya kuingia kwenye chuo cha udaktari. Maandano hayo yamefanyika wakati serikali ikisema kwamba itaanza kuchukua hatua Jumatatu ya kufuta leseni za karibu wanafunzi 9,000 wa udaktari, kutokana na kukaidi amri ya kumaliza mgomo huo, ambao umethiri pakubwa operesheni za kimatibabu nchini.

Waandamanaji hao wamesikika wakiimba pamoja na kutoa maneno ya kukashifu serikali, huku wakiwa wamebeba mabango yakielezea malalamishi yao. Hata hivyo hakuna visa vya ghasia vilivyo ripotiwa. Kufikia usiku wa Alhamisi, madaktari wanafunzi pamoja na wanaohudumu chini ya uangalizi 8,945 kati ya 13,000 waliopo nchini humo, walidhibitishwa kujiunga kwenye mgomo huo, kulingana na ripoti kutoka kwa wizara ya afya.

Serikali imekuwa ikionya kwamba leseni zao zitafutwa kwa miezi mitatu wakati wakifunguliwa mashitaka, iwapo hawangerudi kazi kufikia mwisho wa mwezi uliopita. Korea Kusini ina jumla ya madaktari 140,000.

Forum

XS
SM
MD
LG