Takriban madaktari walio katika mafunzo ya vitendo na wale wanaochipukia 90,000, wamekuwa kwenye mgomo tangu mapema wiki iliyopita, wakilalamikia mpango wa serikali wa kupandisha ada ya masomo kwa takriban asilimia 65.
Mgomo huo unasemekana kuathiri sana shughuli kwenye hospitali kadhaa, wakati baadhi ya matibabu na upasuaji ukisimamishwa. Maafisa wa serikali wamesema kwamba kuongeza idadi ya madaktari ni muhimu kutokana na idadi kubwa ya watu wanaofikisha umri wa juu.
Viwango vya daktari kwa mgonjwa nchini humo ni miongoni mwa vile vya chini zaidi katika mataifa yaliyoendelea. Madaktari waliopo kwenye mgomo wanasema kwamba vyuo vilivyoko haviwezi kumudu idadi kubwa ya wanafunzi wanaojiunga.
Forum