Jeshi la Marekani pamoja na washirika wake limesema kwamba limedungua droni 15 zilizorushwa na Wahouthi wa Yemen wanaoungwa mkono na Iran kwenye bahari ya Shamu na Ghuba ya Aden Jumamosi.
Wakati dunia ikiadhimisha siku ya Kimataifa ya Wanawake Ijumaa Machi 8, nchini Tanzania wanawake wametakiwa kuongeza juhudi zao katika siasa, ili kuhakikisha kuna wingi wa viongozi wanawake nchini.
Somalia na Uturuki zimetia saini makubaliano ya kutafuta mafuta na gesi ambayo yataimarisha zaidi ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, kulingana na maafisa wa nchi zote.
Jeshi la Marekani limesema Shambulizi la kombora lililofanywa na Wahouthi kwenye meli ya biashara ya Bahari ya Sham Jumatano limesabaabisha vifo vya watu kadhaa.
Rais wa Marekani, Joe Biden atatoa hotuba ya Hali ya Kitaifa leo Alhmisi, ambapo anatarajiwa kuzungumzia jinsi alivyoshughulikia uchumi, haki za uzazi, uhamiaji, na vita vya Ukraine na Gaza.
Siku ya Kimataifa ya Wanawake, kampeni ya kila mwaka ya Umoja wa Mataifa ya kuhamasisha juhudi za kuleta usawa wa kijinsia duniani kote, mwaka huu inaadhimishwa kesho Ijumaa, kaulimbiu ikiwa ni "Wekeza kwa wanawake: Ongeza kasi ya maendeleo ."
Maafisa wa serikali ya Iran wanawaweka wanawake chini ya uangalizi mkubwa ili kutekeleza masharti ya kuvaa hijabu kwa lazima, hata ndani ya magari.
Misri imesema Jumatano kuwa imefikia makubaliano na Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF) kuongeza mkopo wa hadi kufikia dola bilioni nane.
Mahakama ya rufaa ya serikali kuu ya Marekani, Jumanne ilikataa kuwajibisha kampuni tano kubwa za teknolojia kwa madai yao ya kuunga mkono matumizi ya watoto katika shughuli za uchimbaji madini ya cobalt katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Walizini wa Pwani wa Ufilipino wamesema kwamba moja ya meli zake imeharibiwa baada ya kugongana na ile ya walinzi wa pwani wa China mapema Jumanne, kwenye bahari ya South China Sea.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilipokeza Tuzo ya Kimataifa ya Wanawake wenye Ujasiri, katika sherehe zilizofanyika Jumatatu katika Ikulu hapa mjini Washington DC.
Maelfu ya wafungwa walitoroka Gereza la Taifa la Haiti, lililopo katika mji mkuu, wakati wa makabiliano ya bunduki usiku wa kuamkoa Jumapili, kati ya polisi wa kitaifa na makundi yenye silaha, afisa mmoja aliiambia VOA.
Mahakama moja ya Bangladesh Jumapili imempa dhamana mshindi wa tuzo ya Nobel Muhammad Yunus aliyehusishwa na kesi ya ubadhilifu wa dola milioni 2.3 za kimarekani.
Wajumbe kwenye bunge la kitaifa la Pakistan, Jumapili wamechagua Shehbaz Sharif, kwa mara ya pili kuwa waziri mkuu mpya wa taifa hilo.
Maelfu ya madaktari waliohudumu kwa muda mrefu, Jumapili wameandamana mjini Seoul, Korea Kusini, ili kuonyesha uungaji mkono kwa wenzao chipukizi, ambao wamekuwa kwenye maandamano kwa karibu wiki mbili.
Muongoza mashitaka wa kieneo amesema Jumapili kwamba takriban watu 170 waliuwawa kwenye mashambulizi dhidi ya vijiji vitatu kaskazini mwa Burkina Faso wiki moja iliyopita, wakati ghasia kutoka kwa wanajihadi zikiendelea kushamiri kwenye taifa hilo linaloongozwa kijeshi.
Ripoti zinasema kuwa mazungumzo kuhusu sitisho la mapigano huko Gaza yanaanza tena Jumapili mjini Cairo, Misri, yakileta pamoja wapatanishi wa Misri na Qatar, wakitarajia kupata majibu kutoka kwa Hamas kuhusu mkakati wao wa karibuni zaidi kuelekea lengo hilo.
Wapalestina 104 waliuawa Alhamisi katika mji wa Gaza wakati wanajeshi wa Israel walipowafyatulia risasi watu waliokuwa wanajaribu kupata chakula kutoka kwa malori ya misaada ya kibinadamu, lakini maelezo kuhusu shambulio hilo baya yanatatanisha.
Umoja wa Mataifa unaisihi serikali ya Taliban nchini Afghanistan kuacha mara moja unyonyaji wa “kinyama” unaofanywa hadharani na kuwachapa watu bakora waliopatikana na makosa ya mauaji na uhalifu mwingine.
Mamlaka nchini Marekani zinasema wana imani kuwa wataweza kukabiliana na vitisho vyoyote vya usalama kuelekea uchaguzi wa rais mwezi Novemba.
Pandisha zaidi