Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 09, 2025 Local time: 21:25

Afghanistan: UN yaisihi serikali ya Taliban kuacha mara moja unyonyaji wa 'kinyama'


FILE - Richard Bennett, U.N. special rapporteur on human rights in Afghanistan, speaks during a news conference in Kabul, May 26, 2022.
FILE - Richard Bennett, U.N. special rapporteur on human rights in Afghanistan, speaks during a news conference in Kabul, May 26, 2022.

Umoja wa Mataifa unaisihi serikali ya Taliban nchini Afghanistan kuacha mara moja unyonyaji wa “kinyama” unaofanywa hadharani na kuwachapa watu bakora waliopatikana na makosa ya mauaji na uhalifu mwingine.

Msemaji wa serikali ya Taliban Zabihullah Mujahid
Msemaji wa serikali ya Taliban Zabihullah Mujahid

Kulaani huko kumekuja wakati mamlaka za Taliban zimewahukumu wanaume watatu kupigwa risasi katika viwanja vya mpira katika miji kadhaa nchini Afghanistan katika wiki moja iliyopita na kushuhudiwa na mamia ya watazamaji.

Katika taarifa iliyotolewa Jumatano, Ofisi ya Haki za Binadamu ya UN mjini Geneva, au OHCHR, ilisema kuwa “imeshtushwa” na unyongaji huo unaofanywa hadharani, ikilalamika kuwa vitendo hivyo “ni aina ya ukatili, unyama au adhabu ya udhalilishaji.”

Taliban imewanyonga hadharani watu watu waliokutwana hatia ya mauaji tangu kuchukua madaraka nchini Afghanistan mwezi Agosti 2021 na pia wamewapiga bakora mamia ya watu, wakiwemo wanawake, kwa kutenda uhalifu kama vile wizi, ujambazi na uzinifu.

Taarifa ya UN imeeleza kuwa adhabu ya kupigwa bakora hadharani hivi karibuni ilifanyika Jumapili iliyopita wakati mvulana wa miaka 12 na mtu mzima walipopigwa bakora hadharani kwa uhalifu wa ukosefu wa maadili huko katika jimbo la mashariki la Laghman.

FILE - Wapiganaji wa Taliban wakifanya doria Kabul, Afghanistan, on Aug. 19, 2021.
FILE - Wapiganaji wa Taliban wakifanya doria Kabul, Afghanistan, on Aug. 19, 2021.

Siku hiyo hiyo, mwanamke na mwanaume waliohukumiwa kwa makosa ya kukimbia nyumbani kwao na uzinifu walipigwa bakora hadharani mara 35 hadharani katika jimbo la kaskazini la Baluchistan.

Adhabu ya viboko pia inakuwa ni aina ya ukatili, unyama au udhalilishaji au adhabu, iliyopigwa marufuku kwa mujibu wa sheria za kimataifa za haki za binadamu,” UN ilitahadharisha.

Imewasihi Taliban wenye msimamo mkali kuhakikisha wanauheshimu kikamilifu mchakato na uendeshaji wa haki wa kesi, hususan upatikanaji wa fursa ya uwakilishi wa kisheria, kwa yeyote anayekabiliwa na mashtaka ya jinai.

Mamlaka zilizopo madarakani Afghanistan zimepuuza ukosoaji kwa mfumo wao wa haki ya jinai, wakisema unaendana na kanuni na miongozi ya Kiislamu.

Taliban wameweka masharti ya jumla kwa haki za wanawake kupata elimu na kushiriki katika shughuli za umma, kuwapiga marufuku wanawake kwenda kwenye viwanja vya mapumziko na gym na kuwakataza wasichana kuendelea na masomo baada ya kumaliza darasa la sita.

Jumuiya ya kimataifa imekataa ombi la Taliban kwa utawala wao kutambuliwa rasmi, wakielezea namna wanavyowatendea wanawake wa Afghanistan na wasi wasi mwingine wa haki za binadamu.

Richard Bennett, mwakilishi wa maalum UN anaye ripoti hali ya haki za binadamu nchini Afghanistan, atazindua ripoti mpya katika mkutano wa Baraza la Haki za Binadamu la UN Alhamisi.


Katika kile kinachoonekana ni kujaribu kukanusha mapema kabla ya ripoti hiyo kutolewa, msemaji mkuu wa Taliban Zabihullah Mujahid aliandika katika mtandao wa X, uliokuwa ukijulikana kama Twitter, kuwa Bennett na wakosoaji wengine wa Magharibi waache “kutumia vibaya” hali ya haki za binadamu Afghanistan na badala yake ijikite na izuiye manyanyaso yaliyoko kwingineko ulimwenguni.
Ripoti ya mwandishi wa VOA Ayaz Gul.

Forum

XS
SM
MD
LG