Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 02:15

Afghanistan yaongeza uagizaji wa mafuta ya Russia licha ya vikwazo vya kimataifa


Kiongozi wa ujumbe wa Russia nchini Afghanistan Zamir Kabulov azungumza na viongozi wa Taliban mjini Kabul. Picha ya maktaba
Kiongozi wa ujumbe wa Russia nchini Afghanistan Zamir Kabulov azungumza na viongozi wa Taliban mjini Kabul. Picha ya maktaba

Utawala wa Taliban wa Afghanistan umeongeza uagizaji wa mafuta kutoka Russia kutoka tani 246,000 hapo 2022, hadi zaidi ya tani 710,000 ndani ya miezi 11 iliyopita, na hivyo kuongeza viwango vya biashara ya mafuta kwa zaidi dola milioni 300, kulingana na maafisa wa Taliban.

Haifahamiki sekta ya kifedha ya Taliban ambayo ina mzigo mkubwa kutokana na vikwazo hivyo imeweza vipi kufanya malipo makubwa ya mafuta kwa Russia.

Vikwazo vya kimataifa vimedumaza biashara za benki na Afghamistan, tangu Taliban ilipochukua udhibiti wa taifa hilo 2021. Marekani hata hivyo ilitoa mwanya wa kuendelea kutolewa kwa misaada ya kibinadamu, mradi isiwe inanufaisha viongozi wa Taliban na makampuni yao.

Mwaka uliopita, maafisa wa Taliban waliingia kwenye makubaliano na Russia ya kuagiza tani milioni 1 za petroli, milioni 1 za dizeli na nusu milioni za gesi ya kupikia. Licha ya kuwa Taliban na Russia wamewekewa vikwazo tofauti na mataifa ya magharibi, hakuna kinachowazuia kufanya biashara pamoja.

Forum

XS
SM
MD
LG