Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 09, 2024 Local time: 13:11

Polisi 10 wauawa katika shambulio Pakistan


Wanajeshi wakiwa katika eneo la Dera Ismail Khan
Wanajeshi wakiwa katika eneo la Dera Ismail Khan

Hakuna mtu aliyedai kuhusika na mauaji hayo lakini tuhuma zimeelekezwa kwa kundi la TTP lililopigwa marufuku huko Pakistan

Maafisa kaskazini magharibi mwa Pakistan wamesema Jumatatu kuwa uvamizi wa alfajiri ulioanywa na wanamgambo umewaua maafisa wa polisi wasiopungua 10 na kuwajeruhi wengine sita kabla ya uchaguzi mkuu baadae wiki hii.

Shambulio hilo lilitokea eneo la kijeshi la Dera Ismail Khan, ambako maafisa waliripoti kuwa kundi la washambuliaji waliokuwa na silaha nzito walivamia kituo cha polisi, wakitumia bundukiza kulenga shabaha na maguruneti na kuwamiminia risasi vikosi vya usalama kabla ya kukimbia.

Polisi wa eneo hilo wamesema operesheni kubwa ya kuwatafuta hivi sasa inaendelea kwa msaada wa vikosi vya Pakistan kuwasaka washambuliaji. Barabara zote zinazoingia na kutoka katika wilaya hiyo zimefungwa.

Hakuna mtu aliyedai kuhusika na mauaji hayo, lakini tuhuma zimeelekezwa kwa kundi la Tehrik-i-Taliban Pakistan au TTP lililopigwa marufuku ambalo mara kwa mara hufanya mashambulizi dhidi ya vikosi vya usalama katika wilaya iliyoko katika jimbo la Khyber Pakhtunkhwa linalopakana na Afghanistan.

Forum

XS
SM
MD
LG