Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 15:27

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan na mke wake wahukumiwa kifungo cha miaka 7 jela


Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan na mke wake Bushra Bibi
Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan na mke wake Bushra Bibi

Mahakama ya Pakistan Jumamosi imemhukumu waziri mkuu wa zamani wa Taifa hilo, Imran Khan na mke wake kifungo cha miaka 7 jela na kulipa faini, ikisema katika maamuzi yake kuwa ndoa yao ya mwaka 2018 ilikiuka sheria, chama chake kimesema.

Ilikuwa hukumu ya tatu dhidi ya Khan wiki hii na inajiri kabla ya uchaguzi mkuu siku ya Alhamisi na haruhusiwi kugombea.

Khan, mwenye umri wa miaka 71 alihukumiwa siku za karibuni kifungo cha miaka 10 jela kwa kuvujisha siri za serikali na miaka 14 jela pamoja na mke wake kwa kuuza kinyume cha sheria zawadi za serikali. Mawakili wake wamesema watakata rufaa katika kesi zote tatu.

Haikufahamika mara moja ikiwa hukumu mbalimbali dhidi yake zitatekelezwa kwa wakati mmoja.

Khan yuko gerezani katika mji wa Rawalpindi, wakati mke wake atatumikia kifungo chake katika nyumba yao ya kifahari iliyoko karibu na mji mkuu Islamabad.

Tayari anakabiliwa na marufuku ya kutoshikilia wadhifa wa utumishi wa umma kwa kipindi cha miaka 10.

Forum

XS
SM
MD
LG