Serikali ya Taliban nchini Afghanistan leo Jumamosi imeishutumu Marekani kwa kuweka vikwazo vipya dhidi ya viongozi wake wawili kwa ukiukaji wa haki za binadamu, ikisema kuwa shinikizo na hatua kali, hazisaidii kutatua matatizo.
Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya wizara ya fedha ya Marekani kuweka vikwazo dhidi ya watu 20 katika nchi tisa, ikiwemo China, Iran na Afghanistan inayotawaliwa na Taliban, kuadhimisha siku ya kimataifa ya haki za binadamu hapo Desemba 10.
Orodha ya majina yaliyotolewa Ijumaa yanayohusiana na Afghanistan walikuwemo Mohammad Khalid Hanafi, mkuu wa wizara ya maadili na tabia wa Taliban, na Fariduddin Mahmood, mwanachama wa baraza la mawaziri la wanaume watupu na mkuu wa Chuo cha Sayansi cha Afghanistan.
Marekani imesema kuwa watu hao wawili wa Taliban walihusika na ukandamizaji wa haki za wanawake na wasichana kwa kulingana na jinsia zao.
Forum