Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 19, 2024 Local time: 15:43

Wanajihadi wadaiwa kuuwa zaidi ya watu 170 Burkina Faso


Wanajeshi wa Burkina Faso wakishika doria
Wanajeshi wa Burkina Faso wakishika doria

Muongoza mashitaka wa kieneo amesema Jumapili kwamba takriban watu 170 waliuwawa kwenye mashambulizi dhidi ya vijiji vitatu kaskazini mwa Burkina Faso wiki moja iliyopita, wakati ghasia kutoka kwa wanajihadi zikiendelea kushamiri kwenye taifa hilo linaloongozwa kijeshi.

Katika siku hiyo hiyo ya Februari 25, mashambulizi tofauti dhidi ya msikiti mashariki mwa nchi na kanisa katoliki upande wa kaskazini, yaliuwa darzeni wengine. Mwongoza mashitaka huyo kwa jina Aly Benjamin Coulibaly amesema kwamba alipokea ripoti kuhusu shambulizi hilo kwenye vijiji vya Komsilga, Nodin na Soroe, vilivyoko mkoa wa Yatenga , Februari 25, ripoti za mwanzoni sikisema kwamba takriban watu 170 waliuwawa.

Mshambulizi hayo yaliacha wengine wengi wakiwa na majeraha, pamoja na kuharibiwa kwa mali, kiongozi wa mashitaka wa mji wa kaskazini wa Ouahigouya ameongeza kwenye taarifa, bila kulaumu kundi lolote. Amesema kwamba ofisi yake imeamuru uchunguzi ufanywe, pamoja na kutoa wito wa kutoa taarifa kutoka kwa umma. Walionusurika mashambulizi hayo wameambia AFP kwamba miongoni mwa waliokufa ni watoto na wanawake.

Forum

XS
SM
MD
LG