Sweden inatarajiwa kujiunga rasmi na NATO katika siku au wiki zijazo, baada ya Hungary hatimaye kutoa idhini yake siku ya Jumatatu – mwanachama wa mwisho kufanya hivyo.
Ofisi ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Jumatatu imesema kuwa jeshi la Israel limewasilisha waraka mbele ya Baraza la Mawaziri la Vita, unaoelezea mpango wa kuwaondoa raia kutoka kwenye maeneo ya mapigano ndani ya Ukanda wa Gaza, pamoja na mikakati ya operesheni katika siku zijazo.
Serikali ya Korea Kusini imewapa madaktari wapya walio katika mgomo muda wa siku nne kurejea kazini, ikisema Jumatatu kwamba watachukuliwa hatua na kusimamishwa kazi pamoja na kufutiwa leseni zao, iwapo hawatafanya hivyo.
Rais wa Ukraine Volodymr Zelenskiy Jumapili alisema ushindi wa Ukraine katika vita dhidi ya Russia unategemea msaada wa nchi za Magharibi, na kuongeza kuwa ana matumaini washirika wao wa nchi hizo za Magharibi wataipa Kyiv makombora ya masafa marefu.
Uchaguzi wa bunge na mitaa nchini Belarus umefanyika Jumapili, licha ya wito wa kuususia kutoka kwa upinzani, ukitarajiwa kuimarisha utawala wa kimabavu wa rais Alexander Lukashenko, ambaye ameongoza taifa hilo kwa karibu miaka 30.
Chama tawala cha Cambodia Jumapili kimejipatia ushindi kwenye uchaguzi wa baraza la Senate, na kwa hivyo kutoa nafasi kwa aliyekuwa waziri mkuu Hun Sen kurejea tena kwenye siasa baada ya kujiuzulu mwaka uliopita.
Jeshi la Ukraine limesema Jumapili kwamba Russia imepoteza wanajeshi 409,820 huko Ukraine ndani ya kipindi cha miaka mbili tangu ilipovamia taifa hilo.
Makampuni katika taifa la Afrika Mashariki, Kenya yanayokabiliwa na changamoto, yanageukia katika teknolojia ya Artificial Intelligence maarufu kama AI ili kupunguza gharama za uzalishaji na matangazo.
Mamia ya waombolezaji nchini Kenya, Alhamisi wamesindikiza jeneza la mwanariadha bingwa wa dunia wa mbio ndefu Kelvin Kitum, wakati lilipokuwa likipekekwa kwenye kijiji chake ambako atazikwa.
Kifo cha kiongozi wa upinzani Russia, Alexei Navalny kimeiweka Russia katikati ya siasa za Marekani na kuongeza shinikizo kutoka kwa Warepublican katika bunge kuiunga mkono Ukraine.
Mcheza soka maarufu aliyewahi kuichezea timu ya Brazil na ile ya Uhispania ya Barcelona Dani Alves Alhamisi amekutwa na hatia ya kumbaka mwanamke kwenye klabu moja mjini Bercelona, na kupewa kufungo cha miaka minne na miezi 6.
Wagombea 15 kwenye uchaguzi ulioahirishwa nchini Senegal wamemshtumu Rais Macky Sall kuwa na nia mbaya na wameapa kuchukua hatua kuhakikisha tarehe mpya ya uchaguzi inatangazwa kwa haraka.
White House inasonga mbele na mageuzi yanayolenga kuimarisha usalama wa mitandao katika bandari za Marekani, baadhi zikiwa pengine tayari ziko hatarini kuangukia kwa wadukuzi wenye mahusiano na China.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy Jumanne amefurahishwa na msaada wa kijeshi wa dola za Marekani milioni 683 kutoka Sweden, ambao umekuja wakati viongozi wa Ukraine wakiendelea kushinikiza kupatiwa msaada zaidi wa kimataifa katika mapambano yao dhidi ya uvamizi kamili wa Russia.
Mama wa marehemu kiongozi wa upinzani wa Russia Alexey Navalny Jumanne, ameomba Rais Vladimir Putin aingilie kati na kuachilia mwili wa mwanawe, ili aweze kuuzika kwa njia ya heshima.
Viongozi wa kijeshi nchini Guinea wametangaza kuvunja serikali bila kutoa maelezo, waksiema watateua serikali mpya, katibu mkuu wa rais amesema.
Taiwan imesema kwamba walinzi wa pwani wa China waliingia kwenye boti moja ya watalii kutoka kisiwa hicho kinachojitawala.
Wafanyakazi wa meli ya mizigo katika Bahari ya Sham walilazimika kuiacha meli yao Jumatatu usiku, baada ya wanamgambo wa Kihouthi kuishambulia kwa kombora la masafa marefu, lililorushwa kutoka Yemen, jeshi la Marekani lilisema.
Serikali nyingi za Ulaya Jumatatu zilisema zinawaita mabalozi na wanadiplomasia wa Russia nchini mwao, kwa kile kinachoelezwa kuwa majadiliano, kufuatia kifo cha kiongozi wa upinzani wa nchio hiyo Alexei Navalny.
Kiongozi wa upinzani wa Tunisia aliye kizuizini Rached Ghannouchi Jumatatu ameanza mgomo wa chakula, akiwa na wapinzani wengine wa serikali, kama njia ya kushinikiza kuachiliwa kwao, mawakili wao wamesema.
Pandisha zaidi