Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 12:37

Kenya: Makampuni yageukia teknolojia ya AI, hofu yazuka soko la matangazo


Mwanamke akitumia mashine ya photocopy katika ofisi ya Google Artificial Intelligence (AI) huko Accra Aprili 10, 2019. - Hiki ni kituo cha kwanza cha AI kufunguliwa Afrika na kampuni ya Google. (Photo by CRISTINA ALDEHUELA / AFP)
Mwanamke akitumia mashine ya photocopy katika ofisi ya Google Artificial Intelligence (AI) huko Accra Aprili 10, 2019. - Hiki ni kituo cha kwanza cha AI kufunguliwa Afrika na kampuni ya Google. (Photo by CRISTINA ALDEHUELA / AFP)

Makampuni katika taifa la Afrika Mashariki, Kenya yanayokabiliwa na changamoto, yanageukia katika teknolojia ya  Artificial Intelligence maarufu kama AI ili kupunguza gharama za uzalishaji na matangazo. 

Hatua hii inasababisha wasi wasi miongoni mwa wasanii na mashirika ya matangazo, ambayo yanahofia kupungua kwa mapato na hasara ya ajira kama AI inaweza kuchukua kazi ambazo wamekuwa wakizifanya siku zote.

Kutokana na kuja kwa atrificial intelligence, makampuni ya Kenya na biashara zimekuwa haraka katika kutumia robot wanaoongozwa na kompyuta kwa shughuli mbali mbali ili kuokoa muda na gharama.

Kartasi Products, ni moja ya makampuni makubwa sana yenye makao yake mjini Nairobi, ni miongoni mwa yale ambayo yanakumbatia teknolojia ya AI. Badala ya kutegemea wasanii wa nje, kampuni hiyo sasa inatumia AI kushughulikia majalada ya vitabu, maandishi na mpangilio – na kupunguza muda wa kudesign kwa theluthi mbili, kutoka takriban miezi mitatu mpaka mmoja.

Allan Omondi ni mbunifu mwandamizi katika kampuni ya Kartasi anaeleza: “…..kwasababu kila kitu kiko ndani ya uwezo wako, kwahiyo unabaini kuwa siyo tu umeokoa muda lakini pia umokoa gharama kwasababu huna haja ya kununua huduma yoyote. Kwahiyo, kwa wakati huu, , unaokoa gharama ambazo tunazipaka kwenye AI, na matokeo yake ni bidhaa kamili.”

David Karega, mkuu wa kampuni ya mawasiliano ya Woodrow kama mkuu wa Mashariki na Kusini mwa Afrika, anasema AI inayasaidia makampuni yanawasiliana na wateja wao.

Anafafanua kuwa: “Katika AI, mashirika, taasisi na makampuni yanaanza kuangalia AI kwa maana ya, “inawezaje kunisaidia kwa wakati huu, ambapo bajeti yangu imepunguzwa, ili kuendelea kufanya mawasiliano yenye ufanisi.’ Nilichokigundua AI inakuwa aina ya mtayarishaji wa thamani, na unaweza kuitumia kuwa mtayarishaji wa thamani kutoka kwa mtazamo wa wakala na kwa mtazamo wa mteja au kampuni.”

Kupitishwa kwa AI kunazua khofu miongoni mwa wasanii na mashirika ya utangazaji kwamba mapato na ajira yataendelea kupungua.

Simon Mwanzia, mkuu wa ubunifu kwa moja ya shirika kama hilo, The Arts Group anakiri kuwa mwenendo na manufaa ya gharama, ingawaje anadhani makampuni huenda yakawa ivuzri zaidi kutegemea watalaamu kushughulikia matangazo yao.

Anaeleza zaidi: “Kazi zote zakubuni zinafanya ndani ya kampuni, kwahiyo ina maana mapatokidogo kwa wakala, kwahiyo kwa hakika kutakuwa na athari. Lakini hatutarajii kuona hali ambapo makampuni yanafanya hivyo kwasababu siku zote tunasisitiza na kujaribu kutetea hilo kwa watu wenye kutaka kulenga kwenye nguvu yao kuu.”

Hivi sasa, program za AI zikitumiwa katika matangazao mara kwa mara huunda vitu fulani na matukio yasiyo ya kawaida ambayo yanahitaji saa nyingi za kuhariri.

Hata hivyo, kampuni ya World Advertising Research Center inasema matumizi yanayofanywa Afrika katika sekta ya matangazo yameshuka kwa asilimia 11.6 mwaka jana – ikiwani ishara kuwa huenda yakaongeza matumizi ya AI.

Ripoti ya mwandishi wa VOA Mohammed Yusuf.

Forum

XS
SM
MD
LG