Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 12, 2025 Local time: 01:48

Mchezaji maarufu wa soka Dani Alves apewa kifungo cha jela kutokana na ubakaji


Aliyekuwa mchezaji wa Brazil na Barcelona.
Aliyekuwa mchezaji wa Brazil na Barcelona.

Mcheza soka maarufu aliyewahi kuichezea timu ya Brazil na ile ya Uhispania ya Barcelona Dani Alves  Alhamisi amekutwa na hatia ya kumbaka mwanamke kwenye klabu moja mjini Bercelona, na kupewa kufungo cha miaka minne na miezi 6.

Jopo la majaji watatu kwenye mahakama ya Barcelona wamemkuta na hatia Alves mwenye umri wa miaka 40 kwa tukio lililofanyika Desemba 31, 2022. Kando na kifungo hicho, mahakama pia imemuamuru kulipa fidia ya dola 162,000 kwa muathirika. Pia amepigwa marufuku kukaribia nyumba yake wala mahala pake pa kazi, huku mawasiliano yote yakisitishwa kwa miaka 9.

Alves ambaye alikuwa mahakamani wakati wa kutolewa kwa hukumu hiyo alionekana mtulivu, kulingana na wakili wake Ines Guardiola. Davis Saenz ambaye ni kutoka upande wa muathirika amesema kwamba wameridhishwa na uamuzi huo, ambao umethibitisha kuwa muathirika alikuwa akisema kweli tangu mwanzo.

Wakili wa muathirika Ester Garcia awali waiki hii alisema kwamba yeye na mteja wake hawatafika mahaka hivi leo, wakati wa kutolewa hukumu hiyo.

Forum

XS
SM
MD
LG